1000410153

Waziri wa ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa onyo kali kwa wananchi wachache waliovamia hifadhi za barabara nchini ambapo ni kosa kisheria na pia ni chanzo cha usumbufu na ajali kwa watumiaji wa barabara.

Bashungwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, leo tarehe 14 Novemba 2023 wakati akikagua upanuzi babarabara ya Chanika ambapo kuna Wananchi wamegoma kupisha eneo la barabara eneo linalotakiwa kujengwa mzunguko wa barabara (round about).

1000410155

“Niwatumie salamu Wananchi wachache wanaovamia hifadhi ya barabara kuwa, sheria ya barabara ya mwaka 1932 inaagiza mita 22.5 toka katikati ya barabara kuwa hifadhi hivyo ilindwe ili kuwezesha Serikali kufanya uboreshaji wa barabara kadri inavyohitajika", amesema Bashungwa.

Bashungwa amewaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS kuhakikisha wanawaondoa wote waliovamia hifadhi za barabara ili kuzilinda na kuziwezesha kudumu kwa muda mrefu.

1000410158

Amesema si vema watu wachache wacheleweshe maendeleo ya Wananchi wakati tayari Serikali imetoa fedha za ujenzi wa barabara za kisasa kwa manufaa ya wananchi wote.

“Wote mliovamia barabara jiandaeni kisaikolojia kwani Serikali hii iko makini kulinda miundombinu yake kwa manufaa ya wote", amesisitiza Bashungwa. 

Kadhalika, Amezungumzia umuhimu wa watanzania kutunza barabara na kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kujenga barabara za kisasa, salama na zinazopendezesha miji ili kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla. 

Nae, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuanzia wiki ijayo watatoa elimu kwa wananchi wa mkoa huo kuhusu umuhimu wa kutunza, kulinda na kuheshimu miundombinu ya barabara, madaraja na hifadhi za barabara kwa manufaa ya taifa.
1000410157
1000410154
1000410156
Share To:

Post A Comment: