Mhadhiri Mwandamizi na mtaalamu wa masuala ya uchumi  katika Chuo cha Uhasibu Arusha IAA Dkt.Cairo Mwaitete ametoa wito kwa watunga sera kuziangalia upya sera wanazozitunga na kuzitengeneza ili ziweze kuendana na wakati unaofaa hasa kwa kuangalia mazingira ambayo sekta binafsi nchini  zinahitajika ziweze kisimamiwa na Watanzania wenyewe.

Akizungumza katika majadiliano ya uchumi wa soko jamii na uchumi shirikishi (Social Market Economy) amesema lengo ni kutaka zualisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi ambapo pia ametoa angalizo kwa watunga sera hao kuwa pamoja na ukuwaji wa kiuchumi kuangalia mamna ambavyo sera zinarahisishaje vijana wanaomaliza masomo kuweza kuanzisha viwanda.

Ameendelea kuwasisitiza watunga sera kuangalia sera za ushirikishwa wa kijamii wa uchumi shirikishi ambao utafanya kutokea kwa matokeo makubwa kwa mtu mmoja mmoja ili kuboresha pato la Taifa.

Aidha amesema lengo la Mkutano huo ni kuhamadisha vijana ili waweze kuwa na manufaa katika uchumi na katika kuujenga lengo kuu likiwa ni kuwataka vijana wajifunze namna ya kuingia kwenye uchumi na kuwa na ujasiri wa kuanzisha viwanda,biashara na kilimo kwa kuzitambua fursa ambazo zinaizunguka nchi.

Naye Mkurugenziwa wa Idara ya utafiti na machapisho kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Mordecai Matto amesema kuwa suala la uchumi shirikishi ni suala la muhimu katika jamii kwani ndiyo uchumu ambao unagusa kila mtu.

Ameongeza kwa kama ilivyo dhamira ya mkutano huo kuweka msisitizo katika uchumi jumishi ambapo kila mtu anapaswa kwa njia moja au nyingine kushiriki kwenye uchumi ambapo amesema kuwa uchumi umekuwa ukikuwa kwa kasi sana isipokuwa katika nafasi ya mtu mmoja mmoja ni chanhamoto, ndiyo maana taasisi za elimu ya juu zimekuwa zikijikita kwenye tafiti ambazo zitasaidia kuhakikisha kila mtu anashiriki katika kuchangia uchumi wa taifa.









Share To:

Post A Comment: