Watumishi sita(6) wa  Kituo cha Afya Njombe Mjini kilichopo Mkoani Njombe wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za wizi wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15.

Baadhi ya vifaa vilivyotajwa kuibiwa ni Mashine ya kupima mkojo, Mashine ya uchunguzi wa wingi wa damu, vifaa vya kuchunguza wingi wa damu na vipimo vya Virusi vya Ukimwi.

Hatua hiyo ni kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka alipofanya ziara katika kituo hicho akiongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na kubaini wizi huo baada ya kuskiliza maelezo ya namna vifaa hivyo vilivyoibiwa.

 Kwa upande wake  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe ACP Mahamoud Hassan Banga amethibitibitisha watumishi hao kushikiliwa kwa ajili ya mahojiano kuhusu tuhuma zinazowakabili na uchunguzi utakapokamilika hatua zingine za kisheria zitaendelea.

Ikumbukwe Watumishi wengine wa nne kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Njombe  walikamatwa na kusimamishwa kazi siku ya jana kwa ajili ya kupisha uchunguzi kutokana na wizi wa Televisheni (TV) 15 zenye thamani zaidi ya  shilingi milioni 11.7 na Kompyuta 2 mali ya hospitali hiyo.






Share To:

Post A Comment: