Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe (Katikati) ambaye ni mgeni rasmi na Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson |Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (Kushoto) wakipokea zawadi kutoka kwa Dkt. Suleiman Kaplan kutoka Uturuki (Kulia) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe akisoma risala wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha.
Dkt. Suleiman Kaplan kutoka Uturuki akiongea na wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe (wa kwanza kulia) akifuatilia matukio wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha. Pembeni yake Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula na Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Elimu, Utafiti na Ubunifu Prof. Anthony Mshandete.
Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia kutoka mataifa ya nje mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia kutoka nchini Tanzania mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia kutoka nchini Tanzania mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-IAST) Novemba 13,2023 jijini Arusha.
.............
Watafiti wa Masuala ya Sayansi wametakiwa kutumia takwimu sahihi za kitafiti zinazosaidia kugundua magonjwa ili zitumike katika kutengeneza dawa zitakazofaa katika kutibu magonjwa mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo Novemba 13,2023 Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Sterolojia unaofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela (NM-IAST) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Ondohuz Mayis cha nchini Uturuki kwa kushirikisha nchi zipatazo 10 ikiwemo Tanzania.
Ameongeza kuwa tafiti hizo za kisayansi na teknolojia zinazogunduliwa zikitumiwa vema zinaondoa changamoto mbalimbali za magonjwa yanayoibuka katika jamii na kuyadhibiti yasilete madhara ambayo huathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Prof. Msoffe anazidi kufafanua kuwa mahusiano ya kitafiti na kigunduzi lazima yazingatiwe zaidi ili kuhakikisha nchi inasonga mbele ikiwemo utoaji wa majibu sahihi ya tafiti yanayoweza kufanyiwa kazi na kuleta majibu sahihi kwa jamii, kilimo na sekta nyinginezo ikiwemo maabara.
Aidha Prof. Msoffe amesema Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zinayofanya vema katika masuala ya sayansi na teknolojia hatua ambayo inasaidia tafiti hizo kukubalika ndani na nje ya nchi.
“Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono maendeleo ya sekta ya Sayansi kwa kuifanya elimu ya juu kuwa ya kimataifa hivyo kuiwezesha nchi kuwa na mahusiano ya kimataifa “Alisema Prof. Msoffe
Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Profesa Maulilio Kipanyula amesema mkutano huo unakutanisha wataalam hao ili kujengeana uwezo katika masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa jamii hususani katika sekta ya afya.
Wakati huo huo, Dkt. Suleiman Kaplan kutoka Uturuki ameeleza kuwa ushirikiano baina ya Chuo cha Ondohuz Mayis na Taasisi ya Nelson Mandela umepeleka mafunzo hayo kufanyika hapo kwa mara ya pili na kuahidi kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali.
Post A Comment: