Na Denis Chambi,  Tanga.

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya nishati na madini imepongeza kasi ya ujenzi kituo kikuu cha mafuta ghafi kilichopo Chongoleani jijini Tanga huku ikiwataka watanzania kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa kuhusu mradi huo  unaotekezwa hapa nchini ukitoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania.

Akizungumza leo November 13,2023 mara baada ya kufanya ziara katika kituo hicho mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. David Mathayo  akiambatana na wajumbe wake  amesema kuwa licha ya  mradi huo ambao una manufaa kwa Taifa hususan kiuchumi  lakini bado wapo baadhi ya watu wa ndani na nje wanajaribu kupotosha kwa kile wanachoeleza kuwa kuna athari za kimazingira zinaweza kujitokeza.

Aidha mwenyekiti huyo ameishauri kampuni ya ECOP ambao ndio wanaotekeleza mradi huo kuangalia namna bora ya kuweza kuendelea kuisaidia jamii katika huduma mbalimbali hususani sekta za elimu,  afya na miundombinu mbalimbali hatua ambayo itakwenda kuunga mkono  jitihada za serikali katika kufikisha huduma karibu na  wananchi hususan wale ambao maeneo yao yanapitiwa na mradi huo .

"Tunafahamu kabisa kwamba huko duniani na hata baadhi ya watu wanasema mradi huu ni mbaya kimazingira lakini sisi wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania una tija kwa taifa letu kwa maendeleo ya uchumi hao wanaosema hivyo pengine wanatumiwa ili waharibu na hawatutakii mema huu mradi una manufaa makubwa sana kwa nchi yetu na ni miongoni mwa miradi michache sana duniani"

"Kwa ujumla katika ziara hii tumefurahishwa  sana na  kasi ya mradi  huu unavyoendelea kutekelezwa lakini tumewapa ushauri katika masuala ya kusaidia jamii inayozungukwa na mradi huu wapo wananchi wengi sana ingalau basi wasaidiwe  kwenye huduma kama kwenye elimu,  maji pamoja na kwamba wanatekeleza lakini wangeweza kuganya zaidi" alisema Mathayo.

"Tunampongez na kumshukuru sana Rais wetu kwa kuendelea kuhakikisha kwamba mradi huu unaendelea kutekelezwa ambao ukifika 2025 utakuwa umekamilika na kazi ya kusafirisha mafuta inaanza na pale ndipo tutaona umuhimu wa mradi huu kwa uchumi wetu na kwa jamii ya watanzania" aliongeza mwenyekiti huyo.

Naibu katibu  mkuu wa wizara ya nishati Athuman Mbutuka ameeleza hatua ambayo kwa serikali imefikia mpaka sasa akisema  wakati ikiendelea kutekeleza majukumu yake yake mpaka sasa tayari shilingi billionb 35  zimelipwa kwaajili  fidia kwa watanzania waliopitiwa na mradi huku zaidi ya wananchi 4228 wakipata ajira katika maeneo ya mradi  huo

"Sisi kama wizara tutahakikisha miradi yote ya maendeleo inakamilika kwa wakati na serikali imeendelea kutimiza majukumu yake katika mradi huu hadi tunavyozungumza mpaka sasa hivi takribani Dolla Million 207 tumeshalipa katika kuchukua hisa zetu ,  mradi umeweza kuajiri 4228 ambao ni sawa na asilimia 91 ya watanzania wote waliopo katika  Mradi kuna makampuni 146 yanayotoa hudum katika mradi na wamepata takriban Billion  355"

"Fidia ilikuwa ni suala kubwa zaidi Serikali kupitia EACOP takriban shilingi Bilion 35 kwa ujumla kayika maeneo mbalimbali ambayo sisi kama tanzania tulikuwa na jukumu la kufanya tumeendelea kutekeleza ipasavyo na tutaenda kuyafanyia kazi maelekezo ya kamati ya bunge" alisema Mbutuka.

Meneja wa mradi huo kutoka  kampuni ya EACOP katika kituo cha Chongoleani Mathieu Fayet amesema kuwa tayari mpaka sasa wameshamaliza kujenga nyumba kwaajili ya wafanyakazi 600 watakaokuwepo kwwnye kambi hiyo kipindi chote cha ujenzi wa mradi huku shughuli nyingine zikiwa zinaendelwa ambapo mpaka sasa zimefiki hatua nzuri

Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi linalotoka Hoima  nchini Uganda kuja Tanzania hadi kituo kikuu cha Chongoleani na urefu wa Kilomita 1443 kutoka Uganda hadi Tanzania ukiwa unatarajiwa kukamili ifikapo mwaka 2025 na kuanza kutoa huduma ya kusafirisha mafuta  huku likiwa linapita katika mikoa 8 ya Tanzania bara.

Menyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. David Mathayo akizungumza na waandishi wa habari  katika kituo kikuu cha mradi wa Bomba la Mafuta ghafi cha Chongoleani yanayotoka Hoima Uganda hadi Tanzania kilichopo jijini Tanga mara baada ya kufanya ziara na kamati hiyo leo November 13,2023.
Naibu katibu mkuu wa wizara ya Nishati Athuman Mbutuka akizungumza na waadhishi wa habari mara baada ya ziara iliyofanywa na kamati ya kudumu ya Bunge katika kituo cha mafuta ghafi kinachojengwa  Chongoleani jijini Tanga.
Meneja wa mradi wa bomba la mafuta ghafi  kutoka  kampuni ya EACOP katika kituo cha Chongoleani Mathieu Fayet akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa kwamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini iliyofanya ziara yake kwa lengo la kujua maendeleo ya mradi huo.

Baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na madini wakiwa katika jiwe la msingi la mradi huo ambalo lilizinduliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.


Share To:

Post A Comment: