Ukame ni hali mbaya ya hali ya hewa ambayo maji yanakuwa hayatoshi kusambaza kwa mahitaji ya mimea na wanyama, pamoja na wanadamu ambao wanaishi mahali hapo. Ni jambo linalosababishwa haswa na ukosefu wa mvua, ambayo inaweza kusababisha ukame wa maji.

Maji ni kitu muhimu kwa Maisha, Ikiwa hakuna maji ukame ni mkali sana na unadumu kwa muda mrefu na matokeo yanaweza kuwa mabaya Kwa hivyo ukame ni moja wapo ya matukio ya kutia wasiwasi sana yanayotokea kwenye sayari, kwa kusimamia visima vya maji tunaweza kuepuka kupata athari zake

Ukame unaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya,kijamii,kiuchumi na kisiasa na matokeo yake ni makubwa,Maji ni moja ya bidhaa muhimu sana kwaajili ya kuishi kwa binadamu pili kwa hewa tu na kupumua.kwahiyo wakati kuna ukame  ambao hauna ufafanuzi ina maana kuwa maji ni machache sana ili kukidhi mahitaji ya sasa hali inayoweza kuwa ngumu na hatari kwa wakazi wa eneo hilo.

Wakazi wa Kata ya Lashaine wilayani Monduli wanakumbwa na janga hili la ukame kwa kukosa maji kwa kipindi kirefu jambo linalopelekea kushindwa kutekeleza mahitaji yao binafsi kama vile kufua,kupika, kuoga na kwa wale wanaotegemea kilimo wanakwama kupata maji kwaajili ya umwagiliaji kutokana na vyanzo vingine vya maji vinakauka.

Judica Elibariki ni mkazi wa Lashaine anayejishughulisha na Kilimo na ufugaji  ambaye anakiri hali ya ukame imesababisha wafugaji wengi kupoteza mifugo yao kwa kukosa malisho na hivyo kuwalazimu kuhamisha mifugo yao nje ya wilaya na hata mkoa ili kunusuru uhai wao.

"Mifugo inakosa chakula,nyasi zinakauka lakini pia mabwawa hayana maji yote unakuta yamekauka sasa kwa hali hii mifugo itaishi kweli?ukame unafanya mifugo kukonda na hata kufa ukienda huko malishoni kipindi cha ukame unakutana na mizoga tu"ameeleza Judica.

“Tunashauri serikali ya Kijiji iwe inapita katika maboma yetu kwa ajili ya kutoa ushauri wa namna gani ya kufuga maana kwa sasa tunateseka sana kwa kweli mifugo imekuwa mingi na chakula hakuna kabisa” aliongezea

Mwanakijiji mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Lesnet Lukumay ameeleza hali hiyo inavyowalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani na mifugo hivyo kujikuta wakitembea umbali mrefu kutafuta maji huku majukumu mengine yakichelewa kutekelezwa ikiwepo kupika chakula cha familia.

“Kuna mwenzetu ana mtoto wa miezi miwili lakini analazikia kumuacha nyumbani na kuja kutafuta maji hali yake hairuhusu lakini kutokana na ukame uliopo hana namna” amesema

“Kwenye kata za jirani tunaona halmashauri wanajitahidi kuwapelekea maji kwa kutumia magari tunaiomba serikali iangalie namna ambayo na sisi tutaweza kuletewa maji mpaka kwa balozi ili na sisi tuweze kuondokana angalau na adha hii wakati tukisubiria mvua inyeshe” aliongezea

Bano Laizer anaeleza kuwa ukame umewasababishia wao na familia zao kuishi kwa shida kwani muda mwingi wanautumia kutafutia mifugo malisho pamoja na Kwenda kutafauta maji kwa ajili ya matumizi yao ya familia ya kila siku.

“Wake zetu wanatakiwa kuoga kila siku ila inawalazimu kukaa aidi ya siku tatu hadi nne bila kuoga kwa sababu hakuna maji Watoto wakati mwingine wanakwenda shule na chafu,tunaiomba serikali itutazame juu ya hili” alisema lazier

“Mabadiliko ya tabia nchi katika eneo letu yametusababishia ukame mkubwa ambao umesababisha maji kuwa shida jambo linalotulazimukutembea umbali mrefu Kwenda kutafuta maji katika moja ya bwawa ambalo lipo zaidi ya kilomita 7” aliongezea

Vitu vyote vilivyo hai vinapaswa kuwa na maji ya kuishi watu wanaweza kuishi kwa wiki bila chakula, lakini siku chache bila maji. unaathiriwa hasa kama usumbufu, hususani kwa hasara za kiuchumi, lakini katika nchi masikini sana matokeo ni ya moja kwa moja zaidi.

Ukosefu wa maji kwa kwa kipindi hiki kirefu kimepelekea ukame kuwaathiri kwa kiwango kikubwa kwasababu eneo limebadilika na kuwa kama jangwa kutokana na upungufu wa mvua za mara kwa mara pamoja na maji kwenye visima, mabomba na kwenye mabwawa kukosekana na kufanya wananchi hao kuwa na taabu kwa kuishi kwa ugumu kutokana na ukosefu wa maji.

Ukame mara nyingi hujenga ukosefu wa maji safi kwa ajili ya kunywa, usafi wa mazingira na usafi wa kibinafsi, ambayo inaweza kusababisha magonjwa mengi ya kuhatarisha maisha tatizo la upatikanaji wa maji ni muhimu kila mwaka, mamilioni ya watu huumwa au kufa kutokana na ukosefu wa upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira, na ukame hufanya shida kuwa mbaya zaidi.

Kutokana na kukosa maji kwa kipindi chote wananchi wamekuwa wakiteseka usiku na mchana katika upatikanaji wake umekuwa ni kwa njia ya maboza tu na yakija yanakuwa ni machache sana hayatutoshelezi kutokana na ukubwa wa familia tulizokuwa nazo.

Ingekuwa tunapata mvua afadhali tungetumia maji hayo kwaajili ya matumizi yetu lakini hata mvua nazo zimekuwa chache kijij kimekuwa kikame jambo ambalo linatupa shida wakazi wa eneo hili.

Ukosefu wa mvua kwa mfululizo na hali ya hewa ambayo huathiri mikoa Fulani na ambayo hutoa majira ya uhaba wa mvua upelekea visima kukauka hata vile vyanzo vya maji tegemezi ubaki bila maji na kutengeneza jangwa.

Hali ya ukame mara nyingi hutoa maji machache sana ili kusaidia mazao ya chakula, kwa njia ya mvua ya asili au umwagiliaji kwa kutumia vifaa vya maji ya hifadhi.

Tatizo sawa huathiri nyasi na nafaka zinazotumiwa kulisha mifugo na kuku, Wakati ukame huzuia au kuharibu vyanzo vya chakula, watu wana njaa, Wakati ukame ni mkali na unaendelea kwa muda mrefu, njaa inaweza kutokea wengi wetu kukumbuka njaa ya 1984 nchini Ethiopia, ambayo ilikuwa matokeo ya mchanganyiko wa mauaji ya ukame mkali na serikali isiyo na ufanisi huku Mamia ya maelfu walikufa kwa matokeo.

Share To:

Post A Comment: