Mazingira maana yake ni jumla ya vitu vyote vinavyomzunguka binadamu pamoja na yeye mwenyewe, viumbe vyenye uhai na visivyo na uhai, vya asili na visivyo vya asili na jinsi vinavyotegemeana. Mazingira ni ghala la kuhifadhi malighafi zote zinazohitajika kuendeleza uhai wa viumbe hai na mfumo-ikolojia.

Binadamu ni sehemu ndogo sana ya mazingira. Mahitaji yote ya binadamu hutunzwa ndani ya mazingira. Mazingira yanahusisha maumbile halisi yawazungukayo binadamu ikiwa ni pamoja na hewa, ardhi, maji, tabianchi, sauti, mwanga, harufu, ladha, vijiumbe, hali za kibiolojia za wanyama na mimea, rasilimali za kitamaduni na masuala ya uchumi jamii na inahusisha mazingira asilia na yaliyoundwa na binadamu na jinsi yanavyoingiliana.

Wakazi wa kwa morombo kata ya Muriet mkoani Arusha wamekosa dampo katika makazi yao wanayoishi kwa muda mrefu na kusababisha kutupa taka hizo kwenye vyanzo vya maji (mito) na kuyatelekeza barabarani ama katika uwanja wa nyumbani kwa mtu.


Wakizungumza na na mwandishi wetu wamemueleza kuwa ukosekanaji wa sehemu ya kutupia taka inawapa wao ugumu katika maisha yao ya kila siku kutokana wanakuwa na taka nyingi na hawana kwa kuzipeleka kutokana na wao kukosa sehem yakuzipeleka kutokana na maeneo wanayoishi kutokuwa na shimo la taka.


Ni kwa muda mrefu hatuna shimo la taka hivyo tunakusanya matakataka tuliyonayo tunayachoma yale yanayochomeka ila taka kama vyakula tunaweka sehem moja mpaka gari la taka litakapoamua kuja ama tunapanda nayo mjini kutafuta jalala na kuyaacha hapo. alisema mama Warda


Ugumu wa utupaji wa taka unapelekea baadhi ya wakazi wa hapa kutupa taka katika vyanzo vya maji ikiwemo mto kidemi kwasababu ukikaa na taka mdaa mrefu haswa za chakula zinaoza na kutengeneza wadudu ambao wanaweza kutusababishia maradhi na ndio maana tunakusanya na kuyapeleka eneo ambalo yateweza kusafirishwa kwa njia ya maji.


Wakazi wa Muriet wamelalamikia upitaji wa gari la kuzolea taka wanaweza kupita hata kwa miezi mitatu mara moja kitendo ambacho sio sahihi maana wakazi wa eneo hilo wakitumia taka kama vyakula na hawana kwakupeleka inakuwa ni tatizo kutokana wanapika kila siku wanaosha vyombo uchafu hatuna kwa kupeleka na hatuezi kuhifadhi ndani wala kuyakushanya mlangoni ili kuepuka magonjwa.


Baadhi ya wakazi wa kwa morombo wengi wao huacha takataka barabarani wakitarajia kuwa gari la taka linawaeza kupita kwa mudaa wowote kwasababu taka hizo zikikaa barabarani zinakuwa kero haswa kwa wapita njia ama wakazi wa eneo hilo na kuhakikisha wanawasumbua wanaopita na gari la taka kuja kukusanya taka hizo.


Winifrida Abbas ni mkazi wa Kijiji cha mlimani ambapo anaeleza kuwa tatizo la mtaa wao kuwa mchafu ni kutokana na watu waliopewa tenda ya kuzoa takataka kushindwa kufanya kazi kwa wakati ingali wanapita kuchukua fedha kiasi cha shilingi 2000 kwa kila nyumba.

“Kama mnavyofahamu asilimia kubwa ya wananchi wa Jiji la Arusha wanaishi huku,wingi wa watu na uzalishaji wa taka unakuwa mkubwa ndio maana unaona takataka zimerundikana kina mahali utasema sijui tupo kwenye dunia gani inatia aibu hebu tusaidieni” Winifrida alisema


Jackson Mjusi ni mkazi wa muriet ambapo amesema magari yanayojishughulisha na ukusanyaji wa takataka yamekuwa hayafiki kwa wakati na wakati mwingine kutofika kabisa hali inayosababisha takataka hizo kuzagaa hovyo ambapo wameiomba serikali iwasaidie waweze kuondokana na changamoto hiyo ambayo ni hatari kwa afya zao.


“Tangu gari lataka lipite ni zaidi ya miezi mitatu jambo ambalo linatupa tabu kwasababu sisi matakataka tunayokila siku pale gari linapokaa miezi mitatu halijapita wanategemea sisi takataka tupeleke wapi?tukitupa barabarani wanasema tunachafua mazingira tukipeleka kwenye vyanzo vya mito wanasema tunaharibu vyanzo hivyo niwapi sehemu sahihi wanataka tupeleke wakati gari la taka halipiti na dampo liko mbali na maeneo yetu” alisema Mjusi


“Wakazi wengine haswa kwasisi ambao tumejenga huku mabondeni unakuta mtu anatoka na uchafu wake nyumbani anakuja kuutelekeza katika uwanja wako wa nyumbani ni jambo ambalo limekuwa kero na unakuwa hujui nani amefanya hivyo tunabaki kulaumiana tukijua kabisa chanzo ni ukosefu wa jalala katika eneo hili.”aliongezea


Tunaomba Serikali ituangalie kwa jicho lingine maana mwisho wa siku tutapata magonjwa ya mlipuko kutokana na kukusanya taka sehemu moja bila kuwa na sehemu ya kupeleka wale vijidudu wanaweza kuingia katika vyakula na kupelekea magonjwa kama kipindupindu kitu ambacho tungeweza kukitatua kwa kupatiwa gari lausombaji wa taka ili kila mwananchi awe salama kiafya.


Tunza mazingira yakutunze, ni usemi ambayo wengi hupenda kuutumia hivyo ni vema kila mwananchi kuhakikisha ana safisha mazingira  yanayomzunguka ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko.


Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa wanaotupa taka inachukuliwa kuwa bidhaa ndogo isiyohitajika ya mchakato wa uzalishaji ambayo inapaswa kuzuiwa ili kuhakikisha kuwa rasilimali za udongo, maji na hewa hazichafuliwi zaidi ya viwango vinavyokubalika

Katika kukabiliana na ushahidi wa kina wa uchafuzi mkubwa unaohusishwa na udhibiti usio na kikomo wa takataka, serikali zimeweka viwango vya taratibu zinazokubalika za ukusanyaji, utunzaji na utupaji ili kuhakikisha ulinzi wa mazingira ila haya yote hayafanyiki kwa wakati licha ya makampuni kuchukua fedha kwa wananchi kwa vigezo vya utunzaji salama wa mazingira kwa njia ya dampo za usafi, uchomaji Pamoja na kupita na gari la kubeba taka hizo.

Ili kuepuka mzigo unaowezekana wa mazingira na gharama zinazohusiana na utupaji taka na kukuza utunzaji kamili wa rasilimali adimu, upunguzaji wa takataka.

Share To:

Post A Comment: