Denis Chambi , Tanga.
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kuwakamata watu tisa wakidaiwa kuwa ni waganga wa kienyeji ambao walikuwa wanajihusisha na ramli chonganishi katika kijiji cha Kivindani kata ya Tongoni Tarafa ya Pongwe wilaya ya Tanga ambapo walikiwa wakifanya ukaguzi katika nyumba zilizokuwa zikisadikiwa kuwa na uchawi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo November 28 , 2023 kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema kuwa wananchi wa kijiji cha Kivindani, kata ya Tongoni Tarafa ya Pongwe wilaya ya Tanga waliwaita waganga hao kwaajili ya kufanya ukaguzi katika nyumba ambazo zilisadikiwa kuwa na uchawi ambao wanakijiji wamekuwa wakilalamika kuwa wakitendewa vitendo vya udhalilishaji kuvuliwa nguo usiku na kuachwa wakiwa watupu.
"Tumefanikiwa kumkamata Hamisi Kombo(46) mkazi wa Kwediboma wilaya ya Kilindi akiwa na wenzake 8 wote ni waganga wa kienyeji ambao wanajihusiaha na ramli Chonganishi wakiwa katika kijiji cha Kivindani kata ya Tongoni Tarafa ya Pongwe wilaya ya Tanga ambao wananchi wa enwo hilo waliwaita waganga hao kwaajili kufanya ukaguzi katika nyumba za kijiji hicho ambazo zinasadikiwa kuwa na uchawi ambao wanakijiji hao walilalamika kuwa wakitendewa vitendo vya uzalilishaji kwa kuvuliwa nguo na kuachwa wakiwa watupu kimazingira wakati wakiwa wamelala usiku , watuhumiwa hao wote wapo nje kwaajili ya dhamana wakati upelelezi wa shauti lao ukiendelea" alisema kamada Almachius.
Aidha katika taarifa nyingine kamanda Mchunguzi amesema kuwa wamefanikiwa kuwakamta watuhumiwa 107 kwa makosa mbalimbali ikiwemo mauaji , wizi wa mifugo unyang'anyi wa kitumia Silaha , kuingia nchini bila kibali pamoja na kupatikana na dawa za kulevya.
"Kati ya watuhumiwa hao watuhumiwa 21 wamekamatwa na Bhangi kilogram 43, Mirungi 124.3 na Heroin 242, watuhumiwa wanne wamekamatwa kwa kosa la kusafirisha raia 7 wa Ethiopia kuingia nchini bila kibali mtuhumiwa mmoja unyang'anyi wa kutumia silaha aina ya Panga na watuhumiwa wengine 74 wamekamatwa na upelelezi unaendelea" alisema Kamanda Mchunguzi.
Alisema watu wa tatu wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9 huku watu nane katika maeneo mbalimbali mkoani hapa wakifariki dunia kutokana na mvua kubwa inayoendelwa kunyesha.
" Kulitokea tukio la mauaji ambapo watuhumiwa ni Rashidi Mwalimu (32) , Siwajui Kigaa (27) na Zuberi Hassan wote wakazi wa kijiji cha Kwandungwa wilaya ya Handeni ambao walihukumiwa kunyongwa hafi kufa kwa kosa la mauaji ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa" alisema
Aidha jumla ya watuhumiwa 41 wamefikishwa mahakamani wakati kesi27 zikitolewa hukumu mbalimbali huku 11 zikiwa zinaendelea ambapo watumiwa watatu ambao ni Justine Kunael (41) , Said Adam (32) na Maliki (38) wakazi wa Handeni wakihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka.
Post A Comment: