Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David Kihenzile ya kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayosimamiwa na Wizara ya Uchukuzi Kwa kutembelea  Tawi la Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kanda ya Kigoma, ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi na Ukarabati wa Meli za Mv Liemba, MT Sangara, Mv Mwongozo na eneo la Katare kitakapojengwa Kiwanda kikubwa Cha ujenzi na Ukarabati wa Meli chenye thamani ya Shilingi Bil 300 ambapo mkataba wake umeshasainiwa

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe David Kihenzile amesema Ukarabati wa Meli ya MV Liemba inayoifanya safari zake kwenye Ziwa Tanganyika unatarajiwa kuanza January, 2024 na utachukua kipindi Cha Mwaka Mmoja Hadi kukamilika kwake.

Mhe Kihenzile ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea, kujifunza na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zake Kwa kutembelea Kampuni ya Huduma za Meli(MSCL) Kwa kanda ya Kigoma, Mkoani humo Tarehe 27 Novemba,2023.

" Mwezi uluopita Serikali iliingia Mikataba ya Ukarabati wa Meli tatu mbili Ziwa Victoria na Moja hii hapa ya MV Liemba, ambapo ukigusa Meli hii unagusa Uchumi wa Wanakigoma,maisha Yao na shughuli zao za Kila siku na ndiyo maana ilipopata changamoto Serikali ikaamua kutenga fedha na tayari tumeshasaini mkataba" amesisitiza Kihenzile.

Ameongeza Ukarabati huo utakaoanza mwanzoni mwa Mwaka ujao unatarajiwa usichukue zaidi ya Mwaka Mmoja ili kazi ianze katika Ziwa Tanganyika na wananchi waendelee kupata huduma kupitia Mali Yao hii kongwe na pendwa.

Mhe Kihenzile amekagua maendeleo ya Ukarabati wa Meli ya Mafuta ya MT Sangara ambayo Ukarabati wake umefikia asilimia 95 na kusisitiza kuwa wakati anakuja kwenye ziara hii Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa alimpigia simu na kumsisitiza kutoa tamko Kwa wasimamizi wa Meli hii ya Mafuta MT Sangara kuhakilisha inakamilika haraka mwezi April ikichelewa mei, 2024.

Ameongeza kuwa Waziri Mbarawa amekuwa akipigiwa simu nyingi na wananchi na wafanyabiashara wa ndani na nje ya Mkoa shauku Yao kubwa ni kuona Meli hii ya Mafuta inafanya kazi ili kuwainua kimaisha,kibiashara na Uchumi wa Maeneo yao na kuongea Pato la Taiga.

Pia Kihenzile ametembelea na kukagua Meli ya MV Mwongozo ambayo imepoteza uimara wake na tayari wataalamu kutoka Chuo Cha Bahari Dar es salaam(DMI) wanaifanyie tathmini kujua ni kiasi Gani kinahitajika ili ianze kufanyiwa matengenezo na kutoa Rai Kwa wataalamu hao kuharakisha mchakato huo ma kuleta mapendekezo Serikalini ili Wizara ijipanhe namna ya kuanza Ukarabati wake.

Vilevile alitembelea eneo la KATABE lenye ukubwa wa Mita za mraba elfu 52 ambapo kitajengwa Kiwanda kikubwa Cha kukarabati na kutengeneza Meli chenye thamani za Shilingi Bil 300 ambapo mkataba wake tayari umeshasainiwa na mda wowote ujenzi utaanza na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia suluhi Hassan imeamua kuweka Kiwanda hicho Mkoani Kigoma ambacho kitawasaidia Watanzania na Nchi jirani na kuifungua Kigoma kibiashara.

Akitoa salamu za Kampuni,Kaimu Meneja wa Kampuni ya Huduma za Meli(MSCL) Kanda ya Kigoma Bw.Allen Butembelo ameishukuru Wizara na Serikali Kwa kuendelea kutenga fedha kukarabati na kujenga Meli mpya kwenye maziwa yetu mchoni na kusisitiza kuwa Kampuni inaendelea kuisimamia wakandarasi wote waliopewa Mikataba Kwa umakini na weledi mkubwa na wamepokea maelekezo yote ya Wizara na Serikali na wanaanza kuyafanyia kazi mara Moja ili miradi yote ikamilike Kwa wakati, ubora na thamani halisi ya fedha

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: