Shirika la Maendeleo la Uingereza (UK-AID) limetoa magari mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 363 kwa Ofisi ta Rais - TAMISEMI na Wizara ya Elimu kwa ajili ya ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za kielemu za Program ya Shule Bora nchini.
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo Novemba 16, 2023 katika Ofisi za TET Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu anayeshughulikia Elimu - Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amepokea Gari la TAMISEMI kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Elimu.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Dkt. Msonde amesema kwa kuwa utekelezaji wa afua mbalimbali unaendelea kwenye mamlaka za Serikali za mitaa magari haya yatasaidia katika ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa afua hizo.
‘Kwa niaba ya Ofisi ya Rais-Tamisemi nichukue fursa hii kuwashukuru FCDO kwa msaada wa gari hizi ambazo zinakwenda kutimiza sehemu ya ndoto za mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb).
Pia Dkt. Msonde amebainisha kuwa, TAMISEMI kama watendaji katika ngazi za Mikoa na Serikali za Mitaa wataendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika yanayoendelea kusaidia katika kuboresha masuala mbalimbali ikiwemo elimu nchini.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo wa Ubalozi wa Uingereza hapa nchini, Bi.Kemi Williams ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano walionesha katika kuhakisha magari hayo yananunuliwa ili kwenda kusaidia katika utekelezaji wa Programu ya Shule Bora utakaosaidia maboresho katika Sekta ya elimu nchini kupitia ufuatiliaji na tamthimini.
Post A Comment: