Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) , Bw. George Kabelwa akiwasilisha mada kuhusu Muundo wa utendaji wa EWURA kwa watendaji kutoka MERA wakati wa kikao kazi kati ya taasisi hizo mbili kilichofanyika ofisi za EWURA Makao Makuu  leo Novemba 13,2023 jijini Dodoma.

Mtakwimu Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bi Rahel Kiula ( wa kwanza kulia aliyesimama) akitoa mada kuhusu uandaaji na utekelezaji wa mpango mkakati wa EWURA wa miaka mitano kwa watendaji kutoka MERA, ambao wamefika EWURA kujifunza kuhusu mipango, ufuatialiaji na tathmini, leo Novemba Novemba, 2023 jijini Dodoma.

Watendaji wa MERA, kutoka kushoto Bw. Charles Kambauwa, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Geoffrey Chilenga, Meneja Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji na Mtakwimu Bi. Olive Moja katika kikao kazi na EWURA kuhusu upangaji, tathmini na ufuatiliaji wa shughuli za udhibiti, kilichofanyika jijini Dodoma, leo 13 Novemba 2023

Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa katika kikao kazi kati ya EWURA na MERA jijini Dodoma leo 13 Novemba 2023

Picha ya pamoja ya Watendaji wa EWURA na MERA wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo watendaji wa MERA, kilichofanyika katika Ofisi za EWURA za Makao makuu jijini Dodoma leo 13 Novemba, 2023

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo tarehe 13 Novemba 2023 imepokea watendaji kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati Malawi (MERA)waliokuja kujifunza namna EWURA inavyofanya kwa ufanisi shughuli za udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw Gerald Maganga, wakati akiwakaribisha watendaji kutoka MERA amesema imekuwa ni desturi ya EWURA kushirikiana na taasisi mbalimbali kwenye masuala ya udhibiti, na kwamba ipo tayari wakati wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi yoyote itakayohitaji kujifunza na kubadilishana uzoefu na EWURA.

“Tumefarijika kuwapokea wenzetu kutoka Malawi kubadilishana uzoefu kwenye utendaji, hii imekuwa desturi yetu na tupo tayari wakati wote kutoa ushirikiano wa hali ya juu, “ anesema Bw. Maganga.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya MERA, Bw. Charles Kambauwa, ameishukuru EWURA kwa ushirikiano na ameeleza kuwa, ufanisi wa EWURA kwenye udhibiti ndio ulioisukuma Mamlaka hiyo kuendelea kupata uzoefu na kujifunza kutoka kwake.

“Tuna hakika tutajifunza namna EWURA inavyoweka mipango, ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za udhibiti na itatusadia kujipanga vyema kwenye majukumu yetu, ni dhahiri tumekuwa tukijifunza mengi kwa EWURA, hilo linajieleza,” amesema Bw. Kambauwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa EWURA, Bw. George Kabelwa, amesema pamoja na mambo mengine, EWURA imeijengea uwezo MERA kwenye uandaaji na utekelezaji wa mpango mkakati, mpango kazi na namna ya kufanya ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za udhibiti kwenye sekta ya nishati.

Ujumbe kutoka MERA umejumuisha Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya MERA, Bwana Charles Kambauwa, Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Bwana Geoffrey Chilenga, Mtakwimu, Bi. Olive Moja na Mchambuzi wa Hesabu, Bi. Chisomo Mandalasi.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: