Watumishi wa Idara ya Manunuzi, Teknolijia ya Habari na Mawasialiano (TEHAMA) na Katibu  katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Njombe  wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa kwa muda kutokana na wizi wa Televisheni (TV) 15 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11.7 na Kompyuta 2 mali ya Hospitali hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka  alipofika katika Hospitali hiyo akiongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa baada ya kubaini wizi huo huku watuhumiwa wa kwanza wakiwa ni watumishi wa hospitali hiyo kutokana mazingira ya siku ya wizi Kontena lenye vifaa hivyo lilifunguliwa kwa funguo.

Hata hivyo baada ya wizi huo haikutolewa ripoti yoyote ya wizi kwenda Jeshi la Polisi badala yake walizungumza na moja ya Mfanyabiashara mjini Njombe ambapo aliwakopesha TV 15 bila makubaliano ya maandishi wakiahidi kumlipa baada ya kupata fedha kupitia kuchangishana.

Watumishi hao watapisha uchunguzi utakaofanyika siku saba na kisha kuandaliwa ripoti ya mkoa ili kubaini  wahusika wa wizi huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Mahamoud Hassan Banga akizungumza na Kings Fm amesema tayari Jeshi la Polisi limeshafungua jarada la uchunguzi ambapo wanawachunguzi watu wa idara  manunuzi na watumishi wengine wanaodhaniwa kuhusika na pindi watakapokamilisha nakubaini waliohusika watawachukulia hatua za kisheria.






Share To:

Post A Comment: