|
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent (wa nne kutoka kushoto) na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji kampuni la Eurochem mara baada ya kikao baina ya pande hizo kando ya jukwaa la wadau wa tasnia ya mbolea Afrika cha Afriqom Fertilizer Club kilichofanyika katika ukumbi wa Park Hyatt Gafden mjini Zanzibar tarehe 1 &2 Novemba, 2023 |
|
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent ((katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Afriqom Mounir Halim (wa pili kushoto) kando ya jukwaa la Afriqom Fertilizer club lililofanyika katika hoteli ya Park Hyatt Garden mjini Zanzibar tarehe 2 Novemba, 2023. Mazungumzo yalilenga kujadili namna pande hizo mbili zitakavyoshirikiana katika kukuza tasnia ya mbolea nchini. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa wa Idara ya Uzalishaji wa Ndani na ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja, Louis Kasera akifuatiwa na Afisa Biashara Mwandamizi, Daniel Maarifa |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent (wa nne kutoka kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya TFRA na Uongozi wa Juu wa OCP Afrika kando ya jukwaa la Afriqom Fertilizer club lililofanyika katika hoteli ya Park Hyatt Garden mjini Zanzibar tarehe 2 Novemba, 2023. Mazungumzo yalilenga kujadili namna pande hizo mbili zitakavyoshirikiana katika kukuza tasnia ya mbolea nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa OCP Tanzania, Hillary Dickson Pato tarehe Mosi Novemba, 2023 |
|
Kaimu Meneja Kitengo cha Uagizaji na Uingizaji Mbolea nchini, Doto Diteba akizungumza wakati wa kikao baina ya TFRA na wawekezaji wa kampuni la AngloAmerican kando ya mkutano uliojulikana kama Afriqom Fertilizer Club uliofanyika tarehe 1&2 Novemba, 2023 katika ukumbi wa Park Hyatt Garden Mjini Zanzibar. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent akiwa katika kikao na mfanyabiashara kampuni la Black Point Agriculture tarehe 2 Novemba, 2023 kando ya Mkutano wa Afriqom Fertilizer Club uliofanyika katika ukumbi wa Park Hyatt Garden mjini Zanzibar. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha na viongozi na watumishi wa Mamlaka walioshiriki mkutano wa Afriqom Fertilizer Club uliofanyika mjini Zanzibar tarehe 1&2 Novemba, 2023. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka, Victoria Elangwa akifuatiwa naKaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Ndani na Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja, Louis Kasera. |
|
Afisa Biashara Mwandamizi wa TFRA, Daniel Maarifa akizungumza jambo wakati wa mdahalo pamoja na wadau kutoka nchi mbalimbali mara baada ya kuwasilisha mada ya ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) katika jukwaa la Afriqom Fertilizer Club lililofanyika mjini Zanzibar |
Na Mwandishi wetu - Zanzibar
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent ametumia ushiriki wake katika mkutano wa wadau wa mbolea wa Afriqom Fertilizer Club kuzungumza na wawekezaji walioshiriki mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Mazungumzo hayo yalilenga katika kuanzisha ushirikiano baina ya wawekezaji na Mamlaka ili kuendelea kuinua tasnia ya mbolea nchini.
Akizungumza na uongozi wa juu wa kampuni la mbolea la OCP Africa mkurugenzi Laurent ametoashukrani kwa uongozi wa juu wa OCP kwa namna kampuni hiyo inavyoshiriki kikamilifu katika kuhudumia wakulima kwa kuwafikishia mbolea pamoja na kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea inayotolewa katika maeneo mbalimbali nchini.
"Tunaelewa kazi kubwa na nzuri sana mnayoifanya ya kusambaza mbolea kwa wakulima lakini pia kuwahamasisha kutumia mbolea tunawashukuru sana" Joel aliongeza.
Aidha, Laurent amewaomba wasambazaji wa mbolea nchini kuwa na imani na serikali katika kulipa gharama ya mbolea ya ruzuku ya mwaka 2022/2023 na kueleza mpaka sasa theluthi mbili ya deni lote imekwishalipwa na kiasi kilichobaki kitalipwa kupitia bajeti iliyotengwa kwa mwaka 2023/2024 wa fedha.
Ameeleza kuwa, kufuatia uwepo wa ruzuku ya mbolea kwa msimu uliopita wakulima walihamasika sana kutumia pembejeo hiyo kwenye kilimo na hivyo bajeti iliyotegwa kutotosheleza maana kiasi kilichotumika ni mara mbili ya bajeti iliyotengwa na kuwasihi kuwa na subra kwani malipo hayo ni lazima yafanyike.
Akizungumza katika kikao hicho Mohamed Hettit Makamu wa Rais wa kampuni la mbolea la OCP ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuja na mfumo wa kidigitali katika kusambaza mbolea.
Amesema, mfumo huo umekuwa namsaada mkubwa kwa wafanyabiashara kwani unasaidia katika kubaini mahitaji ya mbolea nchini kulingana na msimu pamoja na kurahisisha upatikanaji wa takwimu mbalimbali za mauzo.
Kwa siku mbili za mkutano mjini Zanzibar, Mkurugenzi Joel amefanya mahojiano na kampuni tofautitofauti ikiwa ni pamoja na AgroAmerican plc Group, Fertilizer Management and Handling Solutions (BAGTECH), Black Point Agriculture, Afriqom na United Fertilizer Company Limited kujadili namna pande hizo zitakavyoshirikiana katika kuendeleza tasnia ya mbolea nchini.
Post A Comment: