Moja ya jukumu la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni kukagua mbolea zinazozalishwa nchini au kuingizwa nchini kutoka nje ya nchi kabla ya kumfikia mkulima.


Jukumu hilo ni takwa la kisheria na linatekelezwa kikamilifu ambapo kila muingizaji wa mbolea huhakikisha mbolea yake inakaguliwa na kupewa kibali cha kuingia sokoni.

Leo tarehe 14 Novemba, 2023 Maafisa Udhibiti Ubora kutoka TFRA, John W. Sostheness na Levin A. Magera wamefanya ukaguzi katika bandari kavu ya kampuni la Afri- ICD iliyopo eneo la Tazara, Jijini Dar Es Salaam baada ya shehena ya tani 966.28 za Mbolea ya Ammonium Sulphate (SA)21%N kuingizwa nchini na kampuni ya mbolea ya Staco Agrochem.

Katika ukaguzi huo wataalam walijiridhisha kwa kukagua nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kibali cha kuingiza mzigo kutoka TFRA (fertilizer import permit) , Bill permit , Assesment form ya TRA na Taarifa za maabara za Mbolea kabla ya kuja nchini ili kupata taarifa za Mbolea hiyo, kabla ya kuipeleka maabara kwa uchunguzi zaidi wa kikemikali ( Chemical analysis).

Aidha, wataalam hao wamechukua sampuli kwa mjibu wa Sheria ili kupeleka maabara kujua Ubora wa Mbolea kabla haijapelekwa kwa wafanyabiashara hadi kwa mkulima.

Utekelezaji wa jukumu hili unasaidia katika kuhakikisha wakulima wanapata mbolea bora ili waweze kuzalisha Kwa tija.


 

Afisa Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), John W. Sosthenes akijaza fomu maalum  ya kuchukulia sampuli   ya mbolea kwa ajili ya uchunguzi wa Ubora wake   maabara.
 

Afisa Udhibiti ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Levin A. Magera akifunga mfuko uliotumika kuhifadhia sampuli ya mbolea tayari kwa ajili ya kuipeleka maabara ili kudhibitisha ubora wake kabla hazijaingizwa kwa sokoni.
 

Maafisa Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), John W. Sosthenes (katikati walikosimama) na Levin A. Magera (kushoto waliosimama) wakishuhudia ufunguaji wa kontena lililokuwa bandari kavu Afri- ICD eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam tayari kwa  kuchukua sampuli ya mbolea kuipeleka maabara, wa pili kulia ni Afisa Mgomboaji (Clearing and Forwarding Officer) wa Pamyco  Lucas Yonas.

Share To:

Post A Comment: