Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA ) kwa namna inavyotekeleza majukumu yake ya kuzifungua barabara nchini.
“TARURA mnaupiga mwingi kwenye Ujenzi wa madaraja na barabara za mawe,mfikishieni salamu zangu Waziri wa OR-TAMISEMI,Mtendaji Mkuu pamoja na watumishi wote wa TARURA.
Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo tarehe 30 Novemba, 2023 alipotembelea banda la maonesho la TARURA kwenye Kongamano la Kitaifa la 32 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania linalofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mkutano cha Julius Nyerere Arusha (AICC).
Post A Comment: