Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)Denis Rondo akiwa ameambata na wajumbe wa kamati hiyo akiongea mara baada ya kukagua na kuridhishwa na ubora wa miradi yote ya afya wilaya ya Nachingwea
Viongozi wa serikali ya wilaya ya Nachingwea wakiongozana na wajumbe wa kamati ya  kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)
Profesa Kabudi akiuliza swali kwenye jengo la kuchomea taka katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi


Na Fredy Mgunda,Nachingwea.


KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) imeupongeza uongozi wa wilaya ya Nachingwea kwa usimamizi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa ubora unatakiwa kwa mujibu wa miongozo ya serikali

Akizungumza wakati wa ziara ya siku moja katika Hospitali ya wilaya ya Nachingwea,mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)Denis Rondo alisema kuwa wameridhishwa na ubora wa miradi yote iliyojengwa katika hospitali hiyo.

Rondo alisema kuwa majengo yamejengwa kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo imetolewa  na serikali kuu au mapato ya ndani.

Alisema kuwa kamati kwa ujumla inaupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwa kutumia mapato ya ndani kujenga hodi ya maalumu ambayo itasaidia wagonjwa kulazwa kwenye hodi hiyo.

Rondo alisema kuwa kamati imejiridhisha kwa ubora unaotakiwa kwenye ICU ambayo imekuwa moja ya ICU bora Tanzania kutokana na ubora wa jingo lake na vifaa tiba ambavyo serikli ya awamu ya sita imepeleka katika ICU hiyo.

Awali akitoa taarifa kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI),kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Nachingwea DR Ramadhan Mahiga alisema kuwa hospitali ya Nachingwea ilipokea kiasi cha sh. 841,135,130 kwa ajili ya ujenzi wa jingo la OPD,maabara,jingo la kufulia,kichomea taka na mtambo wake lengo likiwa ni kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wanaofika katika hospitali hiyo.

Mahiga alisema kuwa wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kufanya maboresho katika  eneo la upatikanaji wa bidhaa za afya(dawa na vifaa tiba) kupitia bohari ya dawa.

Alisema kwa kipindi cha julai 2021 hadi juni 2022 wilaya ilipokea fedha kiasi cha sh. 392,380,843.11 na kwa kipindi cha julai 2022 hadi juni 2023 wilaya ilipokea fedha kiasi cha sh 705,638,762.92 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma ya afya ambapo ni ongezeko la mara mbili kupitia ruzuku kwenye vituo na kufanya upatikanaji wa bidhaa z afya kuwa alisimia 97   
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: