Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mh. Jacobs Mwambegele akiongoza kikao cha Tume kilichokutana leo Novemba 3,2023 jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine kimemteua Bi. Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama cha Mapinduzi. Uteuzi wa Mbunge huyo ni wakuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Viti Maalum Bi. Bahati Ndingo aliyejiuzulu na kwenda kugombea ubunge katika Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mh. Jacobs Mwambegele (Kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, JAJI wa Rufaa (Mstaafu) Mh. Mbarouk Salim Mbarouk wakati wa kikao hicho cha Tume.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mh. Jacobs Mwambegele (Kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, JAJI wa Rufaa (Mstaafu) Mh. Mbarouk Salim Mbarouk wakati wa kikao hicho cha Tume.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanya uteuzi huo kwa kuzingatia matakwa ya ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (6) na (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Aidha kwa mujibu wa taarifa ya Tume iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadan Kailima, Uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea barua yenye Kumb. Na. CEA.137/400/02A/22 ya tarehe 19 Agosti, 2023 kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoandikwa kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ikiitarifu Tume kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kufuatia kujiuzulu aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Bahati Keneth Ndingo.
Post A Comment: