OR-TAMISEMI


Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ikiwamo sekta binafsi ili kuboresha huduma za afya nchini.

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe  Dkt.Wilson Mahera ameyasema hayo Novemba 23, 2023 alipokuwa akiongoza mkutano wa mwaka wa  wizara za kisekta na wadau unaolenga kujadili jinsi ya kuboresha huduma za afya nchini, jijini Dodoma.

Dkt.Mahera amesema kuwa uwekezaji mkubwa katika miundombinu yakutolea huduma za  afya unatakiwa uendane na huduma bora za afya zinazotolewa katika vituo hivyo.

“Kama mnavyojua serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hasan imewekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, hospitali za rufaa na  ununuzi wa vifaa tiba.Pamoja na hayo yote bado tuna  changamoto ya upungufu wa watumishi, na leo tupo hapa tunajadiliana na wadau jinsi gani tunaweza kutatua changamoto hiyo” amesema.

Dkt.Mahera ameongeza kuwa kuanzia mwaka 2017 serikali imwekeza jumla ya sh.Trilioni moja kwenye afya ya msingi ambapo hadi sasa jumla ya vituo vya afya 530 vinatoa huduma za upasuaji wa mama na mtoto ukilinganisha na vituo 115 viliyokuwapo mwaka 2015.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.John Jingu amesema kuwa serikali itaendeleza mafanikio yaliyopatikana  katika sekta ya afya kwa kuimarisha upatikanaji wa rasirimali watu.

Share To:

Post A Comment: