SERIKALI kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) imekifanyia ukarabati mkubwa Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC) ikiwa ni pamoja na kujenga tanuri la kuyeyushia chuma (Foundry), ukarabati wa miundombinu ya kiwanda na utengenzaji wa mtambo wa kuweka utando katika bidhaa za chuma ili kuzuia kutu (Hot Dip Galvanizing plant).

                                                               

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Hai Mheshimiwa Saashisha Mafuwe Leo Novemba 1, 2023 bungeni jijini Dodoma alilouliza kuwa

"Je, Serikali ina mkakati gani wa kuelekeza Taasisi zake kununua mashine na vipuri katika kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools?" Mheshimiwa Mafuwe


Amesema Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Taasisi zake zinazotumia bidhaa na vipuri vinavyozalishwa na KMTC zinaingia mikataba ya kununua mashine na vipuri kutoka Kilimanjaro Mashine Tools.

Akiuliza maswali mawili ya nyongeza "Je? Serikali haioni Kuna haja ya kuweka mpango mzuri wa kutumia chuma ya Leganga ili kitumike kuzalisha vyuma kwaajili ya taasisi za Serikali?, Serikali imefikia hatua gani kufuatia maombi ya halmashauri ya Wilaya ya Hai ya kupewa eneo kwaajili ya kuanzisha mji mdogo wa kibiashara njia panda ya kwenda Machame?" Mheshimiwa Mafuwe.


Akiendelea kujibu maswali hayo Naibu Waziri Kigahe amesema mikakati ya Serikali ni kuona rasirimali za nchi kuzalisha hasa katika bidhaa za chuma ili Serikali isiendelee kuagiza chuma kutoka nje.



"Utekelezaji wa mradi wa Leganga na Mchuchuma tunaamini ndiyo itakuwa malighafi itakayotumika na kiwanda hiki"Amesema Naibu Waziri Kigahe.



"Tayari Serikali imeshaanza kujadiliana kupitia NDC na wameshaweka 'Master Planning' ili kuona namna ya 'Kuaccommodated' maombi hayo ya Mbunge na Wana Hai ili tuone ni shughuli gani zinazoendana na mahitaji mahususi ya Kiwanda" Amesema Naibu Waziri Kigahe.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: