NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ameridhishwa na teknolojia bora ya mradi wa ujenzi wa Daraja la Ruaha ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 81.8

 Mhe. Adam Kighoma Malima amefika katika kwenye ujenzi wa Daraja hilo Novemba 7, mwaka huu alipotembelea ujenzi huo akiambatana na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ili kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Kilombero.

Hata hivyo Mkuu huyo  amemuagiza Mkandarasi anayejenga Daraja hilo  kukamilisha ujenzi wake kabla au ifikapo Machi 31, 2024 bila kisingizio chochote.

Mradi huu wa ujenzi wa kujenga sehemu ya Barabara kati ya Kidatu na Ifakara kwa kiwango cha lami cha urefu wa km 66.9 na Daraja la Ruaha (Great Ruaha) ni sehemu ya mkakati na juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ili kusaidia wananchi kusafiri bila changamoto na kusafirisha mazao yao katika masoko ya uhakika.

Share To:

Post A Comment: