NA DOTTO MWAIBALE , SINGIDA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amekabidhi takribani Sh.Bilioni 1.6 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya sekta ya afya na elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida.
Hayo yamebainishwa Oktoba 31, 2023 kupitia kikao cha robo ya kwanza cha
Baraza la madiwani cha kujadili mambo mbalimbali ambacho kilikuwa na ajenda
nane.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo. Hussein Simba alisema kati ya fedha hizo Sh.
Milioni 700 zitatumika kununua vifaa tiba.
Alisema fedha nyingine Sh.Milioni 100 zinakwenda kujenga zahanati mbili na
hivyo kuongeza idadi ya ujenzi wa zahanati hizo kufikia nane na kuwa Sh.Milioni
500 zitatumika kujenga jengo la kufulia, jengo la mionzi na dawa katika Hospitali
ya Wilaya.
Simba aliongeza kuwa Sh.Milioni 180 zitatumika kwa ajili ya kuziboresha shule
10 kongwe na Sh.Milioni 128 zinakwenda kujenga bweni kwa ajili ya watoto wenye
mahitaji maalumu.
Alisema Sh.Milioni 544 zinakwenda kujenga Shule ya Sekondari ya Majengo na
zitakazosalia zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa matundu 20 ya vyoo.
Aidha, Simba alisisitiza kwamba halmashauri hiyo imekuwa ikikusanya mara
dufu zaidi ya mapato ikilinganishwa na awali ambapo mpaka sasa kiasi kilicho
kusanywa kinafikia asilimia 54 na kuwa matarajio yao hadi itakapofikia robo ya
tatu watafikisha asilimia 100.
Simba alipongeza juhudi za Serikali kupitia Serikali ya awamu ya sita chini
ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan namna ambayo imeonesha ushirikiano uliotukuka
kwa halmashauri hiyo katika muktadha chanya wa ustawi wa maendeleo ya watu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Leila
Sawe na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo, Jumanne Ismail
walisisitiza halmashauri hiyo kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha zote
zinazotolewa na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
John Mgalula akizungumza kwenye kikao hicho alipokea ombi la Diwani wa Kata ya
Rungwa, Said Yahaya ambaye aliomba asilimia 40 ya mapato yanayokusanywa katika
halmashauri hiyo yawe yanapelekwa kwenye kata kwa ajili ya kutekeleza miradi
anayoibuliwa na wananchi.
Yahaya alitolea mfano wa stendi ya mabasi ya kata hiyo ambapo Mgalula alisema jambo hilo litapitiwa kwenye kamati ya fedha kuona namna ya kufanya na kueleza kuwa kabla ya kamti hiyo kukaa atawatuma madiwani wa viti maalumu kwenda kuangalia mradi huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, John Mgalula akizungumza.
Naibu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jonathan Dule akifutailia jambo kwa makini
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Leila Sewa, akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni, Jumanne Ismail, akizungumza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni Maimuna Likunguni, akichangia jambo.
Waratibu wa vikao wa Halmashauri hiyo wakiwajibika. Kushoto ni Constantine Mihambo na kulia ni Makandaga Magabe.
Diwani wa Kata ya Mgandu, Martin Kapona,akisoma taarifa ya Kamati ya Fedha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, William Masaka, akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.
Diwani wa Viti Maalumu, Utukufu Gwimile na Diwani wa Kata ya Mgandu, Martin Kapona wakipitia taarifa za kikao hicho.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa kwenye kikao hicho.
Wakuu wa idara na wataalamu wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Rungwa, Said Yahaya, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Majengo, Magreth Mwalwayo, akishukuru kwa miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika kata hiyo.
Post A Comment: