Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa katika banda la Ofisi hiyo leo Novemba 23, 2023 Jijini Arusha ikiwa ni Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa juu ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyoshiriki katika Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa Jijini Arusha.

Na; Mwandishi wetu – Arusha
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Joyce Ndalichako amewahimiza wananchi kutembelea mabanda ya sekta ya Hifadhi ya Jamii ili kupata elimu kuhusu sekta hiyo.

 
Prof. Ndalichako amesema hayo leo Novemba 22, 2023 alipotembelea mabanda ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ikiwemo NSSF, PSSSF na WCF katika Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.

 
Amesema, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeendelea kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo wastaafu watarajiwa kuwa na matumizi mazuri ya pesa mara baada ya kupata mafao yao na kuwekeza kwenye miradi yenye tija.
 

Aidha, amewasisitiza wanachi kuwa na utamaduni wa kutunza fedha ili ziwasaidie wanapopata majanga.


Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa Msimamzi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na Mratibu wa Sekta ndogo ya Fedha katika Hifadhi ya Jamii inashiriki pamoja Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha yenye kauli mbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi"

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: