Na.WAF, Dodoma
Naibu Waziri wa Afya leo Tarehe 31, Oktoba, 2023 amekutana na Rais wa Shirika la Kimatifa la Pathfinder Afrika, Bi. Saloucou Zoungrana ambaye amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha kupunguza uwiano wa vifo vya akinamama wajawazito nchini Tanzania.
Bi.Zoungrana ameishukuru Seerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha uanzishaji Programu ya M-mama EmTS nchi nzima.
Aidha ameahidi kuendelea kujitolea kupitia Shirika la Kimatifa la Pathfinder katika kuendeleza afua za afya hususani Afya ya Uzazi kwa vijana, afya ya mama na mtoto na afya ya watu na mazingira
Naye Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Shirika la Kimatifa la Pathfinder
Bi. Zoungrana ameambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Tanzania Shirika la Pathfinder Dkt Joseph Komwihangiro pamoja na Mratibu wa Programu ya M-Mama nchini Tanzania kutoka Shirika la Kimataifa la Pathfinder.
Post A Comment: