Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka watumishi kusimamia miradi ya maji inayotekelezwa eneo la Masuguru-Mchoteka,Nalasi na Mtina wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma Ili iweze kukamilika kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma ya maji kwa urahisi.
Mhandisi Mahundi ametoa maelekezo hayo akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maji inayogharimu fedha kiasi cha shilingi billion 2.8 itakayokwenda kutatua changamoto za wanawake na jamii kwa ujumla kutumia muda mwingi kutafta huduma ya maji.
Pia amewasihi wataalam kujenga tabia ya ushirikishaji wananchi wanapotekeleza miradi ya maendeleo ili wawe na elimu na waweze kulinda na kutunza miundombinu na vyanzo vya maji.
Katika ziara hiyo Mhandisi Mahundi ameongozana na viongozi wa Chama na serikali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro na mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini Daimu Iddi Mpakate baada ya kujionea miradi hiyo wameishukuru serikali kwa kuendelea kufikisha huduma muhimu ya maji kwenye jamii.
Post A Comment: