Na John Walter-Babati

Timu ya Wanawake Mwada Quens imeibuka bingwa wa michuano ya Chem chem Ligi kwa kuichapa Maweni Quens  mabao 4-0.

Wafungaji katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Chem chem Mdori Wilaya ya Babati mkoani Manyara, ni Hellena Shishe aloyetupia mawili , Renalda Emmanuel bao la tatu huku la nne likiwekwa kimiani na Purit Robat.

Licha ya Maweni Quens kupokea kipigo hicho walionyesha uwezo wa kusakata kabumbu lakini bahati haikuwa yao.

Michuano hiyo inafanyika kila mwaka ikidhaminiwa na Chemchem Association kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi na kupinga ujangili katika vijiji 10 vinavyozunguka Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge.


Share To:

Post A Comment: