Na John Walter -Manyara
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Antony Amo(51)Mkazi wa Kijiji cha Endagulda kata ya Eshikesh wilaya ya Mbulu mkoani Manyara ameuwawa na watu wasiojulikana na kisha kuibwa mifugo yake (Ngo'mbe) 40 zenye thamani zaidi ya Million 24.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara George Katabazi ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 30 Mwaka huu ambapo watuhumiwa walimvizia Marehemu akiwa nyumbani kwake.
Amesema watuhumiwa hao walikata kamba za Mlango na kuingia ndani ambapo Marehemu alipojaribu kutoka kuangalia ni kina nani, alichomwa na kitu chenye ncha kali shingoni.
Kwa mujibu wa Kamanda katabazi, chanzo Cha tukio hilo ni kuwania mali ambapo baada ya mauaji waliiba Ngo'mbe 40 wenye thamani ya Shilingi milioni 24 pamoja na mbuzi 48 zenye thamani ya zaidi ya milioni 5.
Hata hivyo kamanda huyo alifika nyumba ya msiba kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki huku akiitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Mpaka Sasa Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa mahojiano huku juhudi za kuipata mifugo hiyo zikiendelea kwa ushirikiano wa Wananchi na upelelezi bado unaendelea.
Post A Comment: