MBUNGE wa Singida Mashariki,Miraji Mtaturu,akichangia leo Novemba 9,2023 bungeni jijini Dodoma mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025 na mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/2025.

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

MBUNGE wa Singida Mashariki,Miraji Mtaturu,ametaja mambo manne yanayowapa nguvu wabunge ya kusimama na kujivunia kuwa watanzania ikiwemo uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na siasa safi chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mtaturu amebainisha hayo Novemba 8,2023,Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025 na mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/2025.

Mtaturu ametaja mambo mengine kuwa ni uwepo wa ardhi ya kutosha inayofaa kwa kilimo na uwepo wa rasilimali watu.

“Ninukuu maneno machache ya Hayati Mwalimu Nyerere wakati tunapata Uhuru mwaka 1961,Mheshimiwa baba waTtaifa alisema kwa… [6:32 PM, 11/9/2023] Mom: MTATURU ASIFU UONGOZI WA RAIS SAMIA NA SIASA SAFI ZA CCM.

MBUNGE wa Singida Mashariki,Miraji Mtaturu,ametaja mambo manne yanayowapa nguvu wabunge ya kusimama na kujivunia kuwa watanzania ikiwemo uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na siasa safi chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mtaturu amebainisha hayo Novemba 8,2023,Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025 na mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/2025.

Mtaturu ametaja mambo mengine kuwa ni uwepo wa ardhi ya kutosha inayofaa kwa kilimo na uwepo wa rasilimali watu.

“Ninukuu maneno machache ya Hayati Mwalimu Nyerere wakati tunapata Uhuru mwaka 1961,Mheshimiwa baba waTtaifa alisema kwamba ili tuweze kupata maendeleo tunahitaji mambo makuu manne ambayo ni watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora,na mambo haya tunayo na tunajivunia nayo,”.amesema.

Amesema katika matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyopita idadi ya watu imeonyesha imefikia Milioni 61 kutoka watu Milioni 44 waliyokuwepo lakini ukubwa wa ardhi uliopo ni mita za mraba 900,000 ambazo ni nyingi sana.

“Nampongeza sana Mh.Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ameamua kuwa champion wa miradi ya maendeleo ya nchi yetu, tumeona katika muda wa uongozi wake amefanya mambo makubwa sana na hata leo tunapata mpango huu tumeona namna ambavyo mwaka uliopita tumetekeleza baadhi ya mambo mengi na yanaonekana kila mahali kwa hakika Tanzania yenye neema inawezekana tunampongeza sana,”.amepongeza.

Amesema kama wabunge wataendelea kumuunga mkono Rais Dr Samia hivyo kumuomba aendelee kukaza mwendo.

“Tunamshuru Rasi wetu kwa kurudisha Tume ya Mipango, tumeona mambo mazuri yaliyowekwa hapa, chombo hiki kilikuwa muhimu sana na Mheshimiwa Rais ameonyesha ana dhamira na amekirudisha kiweze kuisaidia nchi yetu,ahsante sana Rais wetu,”.amesema

Mbali na hilo amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Fedha Dr Mwigulu Nchemba na wataalam wao kwa wasilisho zuri.

Aidha,amempongeza Spika wa Bunge Dr Tulia Ackson kuchaguliwa kuwa rais wa mabunge ya dunia (IPU),na kusema kwa hakika ameiheshimisha Tanzania .

KUHUSU MPANGO.

Akizungumzia mpango huo amesema umeeleza vizuri kwamba utachochea uchumi shindani na shirikishi ikimaanisha kwamba wanaenda kushirikisha watu ambao wamebeba jambo hilo,lakini watu hao hawawezi kufanya peke yao lazima wana rasilimali.

“Rasilimali mojawapo ni ardhi inayofaa kwa kilimo ambacho kimebeba zaidi ya asilimia 80 ya watu wanaojishughulisha na kilimo, mwaka jana pia nilichangia hapa kwa sababu bado naamini kilimo kikifanyiwa mapinduzi makubwa kikiwekezwa vizuri, kikizingatiwa tukapata pembejeo, teknolojia, tukaweka mtaji na maafisa ugani wakawa ni wale walioandaliwa vizuri kitaleta matokeo zaidi,”amesema.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: