Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amehudhuria sherehe ya utoaji wa Tuzo ya Sita ya Balozi wa China nchini Tanzania zilizofanyika jijini Dar es salaam.
Tuzo hizi hutolewa kila mwaka kwa lengo la kutambua mchango wa walimu, wanafunzi na watu mbalimbali katika kusaidia kufundisha lugha ya Kichina.
Aidha, katika hafla hiyo Dkt. Komba alipewa Tuzo ya Mchango Maalumu katika kusaidia ufundishaji wa Lugha ya Kichina nchini Tanzania.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwake na Mhe. Balozi wa China nchini Tanzania CHENI Minglian.
Post A Comment: