Waziri wa Utamaduni,Sanaa na  Michezo Mhe.Darmas Dumbaro ameipongeza timu ya Taifa ya  mchezo wa  golf leo katika ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza mbele ya wanahabari Mhe.Dkt.Darmas Ndumbaro ameanza kuongea mbele ya vyombo vya habari kwa kuanza kuipongeza timu ya golf kwa wanawake kuibuka bingwa kwa nchi sana zilizoshiriki huko nchini Kigali -Rwanda.

"Tanzania hatujawahi kuingia kombe la Dunia na hii ndiyo inaenda kuwa ya kwanza,kushiriki kombe la dunia ,hakika hii ni heshima kubwa kwa nchi lakini pia kwa watanzania  wote kwa kutuletea Kombe nyumbani,"Alisema Mhe.Dkt. Darmas Ndumbaro Waziri wa Sanaa,Utamaduni na michezo.

"Rekodi yetu ni mara ya Nne kwa timu ya mchezo wa golf kwa kutuletea heshima hapa nchini,na sisi kama Wizara tunawakikishia kwamba tutaendelea kuwa nanyi kwa kila kitu,kwa hii heshima kwetu kama watanzania." Alisema Dkt.Mhe. Darmas Ndumbaro Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

" Kwa timu ya Golf tunapenda sana Mhe.Rasi wa chama cha Golf kwa wanawake tunapenda tuwe na timu tatu, ambazo ni U 14, U20 na timu ya Senior ili tuweze kuona ni kwa namna gani tunaweza kuisadia wachezaji wa mchezo wa golf nchini na kuweza kuibua vipaji nchini." Alisema Darmas Ndumbaro Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.

Naye,Kepteini wakati wa kuongea mbele  ya vyombo vya habari ameanza kwa kuongea 

"Kiujumla mchezo ulikuwa ni mzuri na kwa kipekee zaidi nitoe shukurani zangu za dhati kwa Serikali yetu kwa kuendelea kuwa nasi katika mchezo huu wa golf na hakika Mungu ni mwema ,tumeweza kuiwakilisha nchi na kuweza kurudi na kikombe." Alisema Bi. Hawa Wanyeche Kepteini timu ya golf Taifa. 

"Hakika upinzani ulikuwa ni mkali lakini sisi kama timu tulihakikisha kuwa tumeweza kujitoa kwa moyo ili kuweza kuhakikisha kwamba sisi ndiyo wawakilishi pekee kutoka hapa Tanzania, kuweza kuiwakilisha nchi na hakika Mungu ametutangulia na kuweza kuibuka mabingwa kati ya nchi saba ambazo zilishiriki katika mashindano hayo." Alisema Bi.Hawa Wanyeche 

Naye,Rais wa timu ya mchezo wa Golf Bi.Queen Siraki ameanza kwa kuongea na kuwapongeza wachezaji wote wa timu ya yetu ya golf hakika wamefanya makubwa katika mashindano hayo yote kwa takribani nchi saba zilikuwa zinashiriki.

"Hakika mimi nimeweza kujionea mambo makubwa na yenye kufutia zaidi hususani katika wachezaji wetu wa mchezo wa golf kwa wanawake nchini,hakika wametuheshimisha sana kwa kuweza kuonyesha mchezo mzuri kwa takribani michezo yote ambayo wameweza kucheza,wameliheshimisha taifa letu." Alisema B Queen Siraki Rais wa Mchezo wa golf kwa wanawake nchini.

Ameendelea mbele na kuweza kuishukuru Serikali kwa ujumla kwa kuonyesha umoja wa kuwa nao katika safari yao yote walipokuwa nje kuiwakilisha nchi.

"Kipekee zaidi nipende kutoa shukurani zangu za dhati kwa Serikali yetu ikiongozwa na Mhe.Darmas Ndumbaro kwa kuweza kuonyesha umoja kwamba timu yetu imeweza kuwa katika hali ambayo ni nzuri kitu ambacho kilitupa hamasa kubwa hata wachezaji wetu walipokuwa wanacheza." Bi.Queen Siraki Rais wa Mchezo wa wa golf kwa Wanawake nchini.


 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: