Wananchi Mkoani Mara wameaswa kutumia Kliniki ya Ardhi inayoendelea Mkoani Mara kutatua Migogoro inayowakabili badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa wafike ndio wasilishe kero zao.
Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati Tofauti na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma pamoja na Dickson Yohana ambaye ni Kaimu Kamishina wa radhi Mkoani Mara ambapo wamesema kliniki hiyo itatumika kuondoa Migogoro yote katika maeneo yote ambayo yatafikiwa katika Mkoa huo wa Mara.
"Hakikisheni mnafika kwenye hii kliniki katika Mkoa wa Mara hatuhitahiji kabisa kuona Migogoro ya Ardhi inaendelea tunataka Ardhi iwanufaishe wananchi "Dickson Yohana Kaimu Kamishina wa Ardhi Mkoani wa Mara.
Awali akizungumza Bi.Emmy Robert ameishukuru Ofisi ya Kamishina kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kupita katika Wilaya zote kusikiliza Migogoro kisha kutoa suluhisho kwenye maeneo hayo.
"Utaratibu huu ni mzuri sana Ardhi imetufarakanisha wananchi lakini kwa Utaratibu huu Migogoro ya ardhi itaanza kupungua Kabisa kwenye jamii zetu"Alisema Bim Emmy Robert Mkazi wa Bukima.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara Msongela Nitu amewataka wananchi wa wilaya ya Musoma kuacha kuanzisha Migogoro mipya mara baada ya utatuzi huu maana Migogoro hurejesha Nyuma Maendeleo.
Post A Comment: