Daraja la Jordani lililopo Kata ya lemara Mtaa wa levolosi lakamilika kwa Asilimia 70 huku mkandarasi akisema ndani ya wiki mbili zijazo litakuwa tayari kwa matumizi 

Akizungumza wakati wa Ukaguzi wa Ujenzi wa kivuko hicho Diwani wa Kata ya lemara Naboth Silasie amesema ni faraja kwao kupatikana kwa kivuko cha jordani kwani  kinaunganisha mitaa miwili ambapo ni Elikirowa na Mtaa wa olepolosi

Amesema kuwa upatikanaji wa kivuko hicho ni Kutokana na jitihada za kujenga hoja kwenye ngazi ya Mtaa na Jimbo ambapo mahitaji yalikuwa ni kujengwa kwa madaraja matatu ambapo ni Daraja la Mungu, Daraja la Jordani na Daraja la Elikirowa

Amesema kuwa kivuko cha Daraja la Mungu tayari kimekamilika ambapo Shilingi Milioni sabini na tano  kutoka TASAF zilitumika kwenye Ujenzi huo

Sambamba na hilo Naboth amesema Kwa upande wa kivuko cha Jordani fedha zilizotolewa kutoka katika mfuko wa Jimbo ni Shilingi Milioni kumi ambapo zinatumika kukamilisha Ujenzi huo

Amesema hapo awali wakazi wa maeneo hayo walikuwa wanashindwa kuvuka hasa watoto na waendesha pikipiki ambao iliwalazimu kuzunguka upande wa pili kwani ukifika wakati wa Mvua eneo hilo huwa halipitiki

Pia amewaomba wananchi wa Mtaa wa levolosi kukipokea kivuko hicho huku akitoa rai kwa wakazi wa maeneo hayo kuonyesha ushirikiano katika kutunza kivuko hicho kwani Serikali haiwezi kufanya Kila kitu bila ya ushirikiano na wananchi

Nae Mwenyekiti wa Mtaa wa levolosi Rashida Shabani amesema kivuko kilichokuwepo hapo awali kilikuwa ni mbao ambapo wananchi na watoto walikuwa wanaanguka wakati wakipita katika Daraja hilo

Amesema juhudi za Diwani wa Kata hiyo Naboth Silasie zimezaa matunda kwani Daraja hilo mpaka Sasa limefiki asilimia 70 ingawa changamoto iliyopo  eneo hilo ni tindiga hivyo kadri wanavyozidi kuchimba udongo unaanguka naMaji yanatoka mengi huku akitoa rai kwa mkandarasi kuongeza kazi kukamilisha kivuko hicho kwani tunaelekea msimu wa mvua nyingi

Nae Mkandarasi anaejenga Daraja hilo la Jordani amesema KAZI imefikia asilimia 70 na asilimia 30 imebakia kufunika juu Ili watu waanza kupita

Amesema kwa asilimia zilizobaki atatumia wiki mbili kukamilisha kazi yote kwani vifaa vyote vipo huku akiomba kuletewa mapema vifaa vilivyobaki kwa wakati.




























Share To:

Post A Comment: