Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ujenzi wa mradi wa skimu ya umwagiliaji uliopo Kijiji cha Msingi Kata ya Msingi wilayani Mkalama mkoani Singida Novemba, 14, 2023.. 

...............................................................

  Na Dotto Mwaibale, Singida 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa skimu ya umwagiliaji uliopo Kijiji cha Msingi Kata ya Msingi wilayani Mkalama mkoani Singida ambao serikali imetoa zaidi ya Sh. Bilioni 34. 

Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Mkalama Mwenyekiti wa kamati Daniel Sillo  aliipongeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Raymond Mndolwa kwa kazi kubwa inayoifanya ya kukamilisha miradi hiyo ya ujenzi wa mabwawa ambayo ni muhimu kwa Taifa ukiwemo mradi huo wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kata ya Msingi Mkalama. 

Sillo alisema kukamilika kwa mradi huo  kutaongeza pato la  mtu mmoja mmoja na  taifa kwa ujumla na kuwa mradi huo na mingine yote itakapo kamilika inakwenda kuchangia ongezeko la fedha katika bajeti ya Serikali. 

Sillo alisema miradi hiyo inatekelezwa kwa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anataka kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa wananchi kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Aidha, Silo aliwataka wananchi wasijenge kwenye eneo la mradi hasa kwenye mashamba yanayotarajia kulimwa kwani mradi huu ukikamilika utawanufaisha wao kwa kulima zaidi ya mara moja kila mwaka .

Sillo aliiomba Wizara ya Kilimo hasa Tume ya Taifa ya  Umwagiliaji kusimamia vizuri mradi huo na kukamilika kwa wakati ili uwe na tija kwa wananchi na Taifa.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amempongeza Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji . Raymond Mndolwa kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji. 

Silinde alisema serikaki inataka wananchi walime si kwa kutegemea mvua na kwamba mradi huo utakapokamilika utaongeza pato la mwananchi sababu atakuwa anavuna zaidi ya mara mbili kwa mwaka na pia itaongeza pato kwa halmashauri na usalama wa chakula nchini.

Akizungumzia suala la wananchi kuanza kujenga katika mashamba, Silinde alisema ni kwasababu wanafahamu nini kinakwenda kutokea na kuwataka waache serikali itengeneze miundombinu ya mradi huu kwani lengo la serikali ni kuondokana kwenye kilimo cha kienyeji kuja kwenye kilimo cha kisasa chenye tija.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Raymond Mndolwa, alisema ujenzi wa mradi huo utakapokamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya wakazi 12,000 wa vijiji vinne vilivyopo Kata ya Msingi.

Aidha aliieleza kamati hiyo kuwa wananchi wameanza kujenga nyumba kwenye eneo la mradi huo hivyo kuanza kupoteza eneo la kilimo ambapo aliomba eneo la uwekezaji thamani yake ni vema likabaki lile lile vinginevyo manufaa ya uwekezaji itakuwa ni bure.

Mndolwa aliwaomba viongozi wa serikali ya wilaya na mkoa iingilie kati suala hili kwa kuwazuia wananchi wasiendelee kujenga mashambani kwani Sh.Bilioni 34 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mradi huu ni fedha nyingi.

Hata hivyo, Mndolwa alisema tume itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na kuwa miradi yote inayojengwa itakamilika kwa wakati na serikali inaendelea kutoa fedha kwa aajili ya utekelezaji.

Awali Mkurugenzi wa Idara ya Ukarabati na Ujenzi wa  Miundombinu, Mhandisi Fuko Koyoya, alisems mradi huu ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 utawanufaisha wakazi 12,000 wa vijiji vinne vya Ishinsi, Ndurumo, Msingi na Kidi vilivyopo Kata ya Msingi tarafa ya Kinyangiri ambao watalima mazao ya mpunga,mahindi na mbogamboga Kwa misimu miwili hadi mitatu kwa mwaka. 

Alisema shughuli zitakazofanyika katika mradi huu ni ujenzi wa bwawa lenye ujazo wa Lita 1,875,000, ujenzi a mifereji ya umwagiliaji yenye kilometa 19.12, uchimbaji wa mifereji ya matupio yenye urefu wa kilo mita 42.539, uchimbaji wa mifereji ya kuingiza Maji mashamba yenye urefu wa jumla ya kilometa 34.778.

Shughuli nyingine zitakazofanyika ni ujenzi wa barabara za mashamba zenye urefu wa kilomita 36.1, kusawazisha ekari 2,000 za mashamba,ujenzi wa kilomita nane za barabara na makaravati sita kuelekea ndani ya mradi na ujenzi wa vigawa Maji 14,vipunguza mwendo,viumbo angalizi 90,vipitisha maji 90,makaravati 14 pamoja na vivuko nane.

Mradi huo ambao umeanza kujengwa Julai Mosi mwaka huu unatarajia kukamilika Disemba 14, 2024.

Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, akisisitiza jambo mbele ya kamati hiyo.


Mkurugenzi wa Idara ya Ukarabati na Ujenzi wa  Miundombinu, Mhandisi Fuko Koyoya, akitoa taarifa ya mradi huo.

 Naibu Waziri wa Kilimo,  David Silinde, akizungumza wakati wa ziara hiyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Daniel Sillo, akizungumzia mradi huo.


Mjumbe wa kamati hiyo, Zaituni Swai, akijitambulisha.


Mjumbe wa kamati hiyo, Rashid Abdalla Rashid, akijitambulisha.



Mjumbe wa kamati hiyo, Reuben Kwagilwa, akijitambusha.

Mjumbe wa kamati hiyo, Shally Raymond, akizungumza.

Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Francis Isack, akishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo ambao ni muhimu kwa wananchi na taifa.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali (kulia) akizungumza wakati akiwakaribisha wajumbe wa kamati hiyo.

Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ziara hiyo wilayani Mkalama.

Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ziara hiyo wilayani Mkalama.

Safari kuelekea ulipo mradi huo ikifanyika.

Muonekanao wa ujenzi wa skimu hiyo ya umwagiliaji.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: