Na Mwandishi wetu - Mtwara
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe Suleiman Kakoso amepongeza jitihada zilizofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini(TPA) za uendelezaji wa bandari ya Mtwara.
Mhe kakoso ameyasema hayo wakati wa muendeleo wa ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini(TPA) kwa kutembelea gati za bandari ya Mtwara likiwemo gati linalotumika kusafirisha korosho,kutembelea mahali panapojegwa bandari mpya ya mizigo ya Kisiwa Mgao sambamba na kutembelea uwanja wa ndege wa Mtwara mkoani humo tarehe 13 Novemba,2023.
Kakoso amemshukuru Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kwa jitihada kubwa alizozifanya mkoa wa Mtwara kwa kutoa fedha kwa TPA zilizotumiwa kujenga gati jipya lenye urefu wa mita 3,500 ,ufungaji wa mitambo ya kupakia na kupakua makasha,ujenzi wa mzani wa upimaji bandarini na uboreshaji wa miundombinu ya kutoka na kuingia bandarini ambavyo vimeongeza ufanisi wa bandari ya Mtwara.
“uwekezaji ambao umewekezwa na serikali kwenye bandari hii ni mkubwa sana tumeona ufungwaji wa mitambo, na miundombinu wezeshi imekamilika tunaishukuru Wizara ya Uchukuzi kwa jitihada zilizofanywa hapa ambapo pia kunajengwa bandari mpya itakayohudumia mizigo ya makaa ya mawe na sarujii ili kuepusha uhalibifu wa mazingira ambao upo kwenye maeneo haya ambako wananchi wanatumia bandari hii na wanaishi Jirani na bandari” amesisitiza Kakoso
Amesema kamati imejiridhisha na kuangalia jitihada ambazo zimefanywa na TPA kile ambacho kiinasemwa ni tofauti na uhalisia ambao wameona ambapo kamati imeona makasha mengi yako kwenye eneo la bandari na kuna hatua kubwa za maendeleo na maboresho ambazo kamati hiyo imeona ambavyo imeongeza ufanisi wa utoaji huduma na mapato.
Ameongeza kuwa huko nyuma kulingana na idadi iliyotolewa na mamlaka idadi ya mizigo ilikuwa kidogo lakini kwa sasa imeshuhudiwa mapato makubwa ya bandari ya Mtwara mpaka kufikia Bil 35 kwa mwaka 2022/2023 na kuna uwezekano wa kufikia Bil 40 sababu mzigo bado ni mkubwa unaohitaji kuhudumiwa na kutoa wito kwa wananchi wa Mtwara,Lindi na Ruvuma kuitumia bandari ya Mtwara ili kuongeza uchumi wa nchi na mkoa.
Awali Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kupokea salamu za mkoa pia ilitembelea na kukagua maboresho ya Uwanja wa ndege wa Mtwara ambao umekamilika kwa kuongezwa eneo la kuruka na kutua ndege kwa mita 2,840 na kufungwa taa zinazoruhusu ndege kutua usiku kinachosubiriwa ni vitendea kazi ili wananchi waanze kupata huduma za ndege Zaidi na kuwataka ATCL kufikiria kuanzisha safari mkoani Mtwara.
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David Kihenzile ameishukuru kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa kutembelea uwanja wa ndege wa Mtwara, inakojegwa bandari ya mizigo ya kisiwa mgao na bandari ya Mtwara na kusisitiza kuwa mambo yote ambayo kamati imeyabaini na kuyatolea maelekezo Wizara imeyachukua na inakwenda kuyachakata na kujipanga kuyafanyia kazi kwa haraka.
Akitoa maelezo ya awali Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandar Nchini(TPA) Mha Juma Kijavara amesema bandari ya Mtwara ni miongoni mwa bandari tatau zilizoko kwenye mwambao wa Bahari ya hindi zilizopo chini ya TPA.
Kijavara amesema kutokana na maboresho Bandar ya Mtwara imepata gati jipya lenye mita 3,500 lenye uwezo wa kuhudumia tani 65,000 na bidhaa zinazohudumiwa Zaidi ni korosho,makaa yam awe na saruji zinazokwenda Tanzania visiwani,Comoro,msumbiji, India, aasia na Bara ulaya ambapo mwaka 2021 bandari ilihudumia meli 64 huku mwaka 2023 ikihudumia meli 213 na mizigo tani 177,338 mwaka 2021 mpaka tani Mil 1.6 mwaka 2022 likiwa ni ongezeko la asililia 93 huku mapato yakiongezeka kutoka Bil 11 mwaka 2021 mpaka Bil 35 mwaka 2022/2023
Post A Comment: