Mkuu wa wilaya ya Same  amefanya ziara na kuzungumza na wafanyabiashara mbalimbali kwenye wilaya ya Same kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo, pia kuangalia utekelezaji wa Sheria ikiwemo wajibu wa msingi wa kulipa kodi.


Kwenye wilaya ya Same tuna zaidi ya wafanyabiashara 1,300 waliosajiliwa Mamlaka ya mapato TRA lakini ni wafanyabiashara 180 Pekee walio na mashine za EFD ambapo pamoja na Mambo mengine maagizo yangu kwa TRA ni kusimamia wafanyabiashara wote wanaopashwa kuwa na mashine za EFD kuhakikisha wanakua na machine hizo katika Kipindi cha mwezi mmoja.alisema Dc Kasilda


Mgeni. aliendelea kusema tunapo sisitiza matumizi ya mashine za EFD ni kutaka kuwa na urahisi kuwawezesha wafanyabiashara kulipa kodi stahili kulingana na Biashara wanazo zifanya kwakua mwananchi anapo nunua bidhaa yoyote na akapewa Risiti ndipo anapata nafasi ya kushiriki kuchangia maendeleo ya nchi yake moja kwa moja kwakua fedha hizo hizo ndizo zinarudishwa kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo tunayo ishuhudia kwenye maeneo yetu ikiwemo ujenzi wa barabara, Madarasa, Zahanati nk. 


Pia  niendelee kuwaomba wakazi wa Wilaya ya Same tuendelea kutii maelekezo ya viongozi wetu, kutimiza wajibu wetu kwa kutoa Risiti unapo fanya mauzo na kudai Risiti kwa kila bidhaa tunayo inunua kufanya hivyo sio tu tunatumia haki yetu bali ndio uzalendo wenyewe kushiriki kwenye upatikanaji wa mapato. Alisema Kasilda Mgeni mkuu wa wilaya ya Same




Picha mbalimbali za Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni. Akikagua risit kwenye Duka wakati akiwa kwenye ziara na kuzungumza na wafanyabiashara Mbalimbali Wilayan Same




 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: