Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
Post A Comment: