Wauzaji wa Vifaa vya ujenzi Nchini Dar Ceramica Centre watoa Punguzo la bidhaa kwa asilimia sita Mkoani Arusha
Akizungumza wakati wa kuzindua duka hilo la vifaa vya ujenzi Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema wananchi wanapowekeza fedha zao katika Ujenzi lengo hasa ni kuweza kupata vifaa vilivyo bora ili uwekezaji huo ulete thamani kwa wananchi
Amesema kuwa uwepo wa kampuni hio Jijini Arusha utakwenda kutoa ajira kwa wananchi na kwa mafundi Ujenzi ambao watatumia vifaa hivyo katika shughuli zao.
Sambamba na hilo Mongella ametambua mchango wa Dar Ceramica Centre katika kuchangia ulipaji Kodi ambazo zinachangia katika mfuko wa Serikali ambao hupelekea maboresho ya huduma za kijamii Nchini ikiwemo Barbara,huduma za Afya,Maji,Umeme na Elimu
Mongella amesema wao kama Serikali ya Mkoa wa Arusha wapo tayari kuwaunga Mkono na watakuwa mabalozi wa kampuni hio kwani sio tu wamewekeza kupata faida bali watakuwa ni Wadau wa kubwa katika kuchangia maendeleo ndani ya Mkoa wa Arusha
Nae Mkuu wa Masoko wa Dar Ceramica Centre Raymond Nkya amesema wao wamejikita kutoa huduma Bora kwa wananchi ambapo kwa Sasa wameifikia mikoa Saba wakitoa huduma ya vifaa vya ujenzi vyenye ubora wa Hali ya juu
Nae Jane phidelice amesema wamekuwa wakitumia vifaa vya ujenzi kutoka kwa kampuni hio tokea mwaka 2006 kwani kampuni anayofanyia kazi inajihusisha na maswala ya ujenzi, amesema Kutokana na huduma hio ya duka kusomezwa karibu Yao itawawezesha kuvipata vifaa hivyo kwa wakati
Pia ametoa ushauri kwa wakazi wa Arusha hasa makampuni ya Ujenzi kuwa vifaa vinavyouzwa na kampuni hio vina ubora wa Hali ya juu kwani vinadumu zaidi ya miaka ishirini vikiwa na upya wake tofauti na vifaa vingine ambavyo ukinunua lazima ndani ya miaka miliwi urudi kununua tena.
Post A Comment: