Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Lindi Alhaji Hassan Jarufu akiongea mara baada ya kamati kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya ya Nachingwea ambayo imetekelezwa kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Lindi Alhaji Hassan Jarufu akiongea mara baada ya kamati kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya ya Nachingwea ambayo imetekelezwa kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Lindi kimeupongeza uongozi wa wilaya ya Nachingwea kutekeleza miradi ya maendeleo Kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa serikali pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.


Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya utekelezani ya CCM mkoa wa Lindi, mwenyekiti wa CCM Lindi Alhaji Hassan Jarufu alisema kuwa wametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya ya Nachingwea na kujionea namna ambavyo imetekelezwa kwa ubora wa hali ya juu jambo ambalo linalowapa faraja wananchi wa Nachingwea.


Jarufu alisema kuwa miradi yote imetekelezwa kulingana na thamani ya fedha ambazo serikali imekuwa ikitoa katika kuleta maendeleo kwa wananchi ambao ndio wamekiwa chama hicho madarakani.


Alisema kuwa usimamizi mzuri kutoka Kwa viongozi wa serikali ya wilaya ya Nachingwea ndio unaosababisha kutekeleza miradi yote kwa ubora kulingana na thamani ya fedha husika ya mradi.


"Nachingwea mnabahati sana maana viongozi wenu ni watoto wa viongozi wa zamani wa serikali na chama cha mapinduzi,mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ni mtoto wa mzee Nassor Moyo na mkurugenzi wenu Chionda Kawawa ni mtoto wa mzee Kawawa ndio maana mnaona Nachingwea sasa inapaa kimaendeleo"alisema Jarufu 


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan Kwa kupeleka fedha nyingi katika wilaya hiyo.


Moyo alisema kuwa serikali ya wilaya hiyo imejipanga kusimamia vililivyo fedha zote kutoka serikali kuu na fedha za mapato ya ndani zinatumika vizuri kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Nachingwea.


Alisema kuwa uongozi wa wilaya ya Nachingwea unaomba viongozi wa CCM kufikisha salama Kwa Rais Dr Samia suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mikubwa na midogo katika wilaya ya Nachingwea 

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: