Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai (kushoto) akipokea tuzo ya mlipa kodi bora.
MSD Yatwaa Tuzo Ya Mlipakodi Bora 2023
..............................................
Na Mwandishi Wetu
BOHARI ya Dawa (MSD), imetwaa tuzo ya Mlipakodi
Bora kwa mwaka 2023 ya Mamlaka ya Kodi Tanzania.
Tuzo hizo zimetolewa usiku wa Novemba 24, 2023 katika hafla maalum
ya wiki ya Mlipakodi zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijiini Dar es
Salaam ambako Bohari hiyo imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha
WalipakodiWalipakodi wa Kati kwa Mkoa wa Kikodi wa Temeke.
Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD,
Mavere Tukai amesema ushindi huo una maana kubwa kwa Bohari hiyo na Watanzania.
Amesema MSD ambayo ni moja ya Taasisi za
kimkakati za Serikali inayohusika na kuzalisha, kununua, kutunza na kusambaza
bidhaa za afya kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali
nchini inafuata taratibu, sheria na miongozose ikiwa ni pamoja na kulipa kodi
stahiki.
"Maendeleo yoyote ya nchi yanategemea kodi
zinazolipwa hivyo ni vyema kila mlipa kodi akalipa kodi stahiki ili kuwezesha
muendelezo wa biashara na kuimarisha
maendeleo kwa mustakali wa ustawi wa jamii, " ameongeza Tukai katika hafla
hiyo ambako mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Tukai, MSD sasa iko
katika mkakati wa kujiendesha kibiashara hivyo hatua ya kulipa kodi kwa
utaratibu uliowekwa hadi kutambuliwa ni fursa ya kuaminika kwa wadau wetu
katika huduma tunazotoa.
Awali Mkurugenzi wa Elimu wa Mlipakodi na Mawasiliano, Richard Kayombo alisema vigezo vilivyotumika kupata washindi ni kulipa kiasi kikubwa cha kodi na hiari pamoja na kutunza kumbukumbu vizuri
Post A Comment: