Na Denis Chambi,  Tanga.

BINGWA wa michuano ya  kombe la Odo Ummy Super  Cup inayotarajiwa kuzishirikisha timu za vijana kutoka kata 27  ikidhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalim anatarajiwa kuondoka na Kombe ,  jezi seti mbili pamoja na kitita cha shilingi Million tatu.

Mbunge huyo ni kama amedhamiria kumwaga maokoto kwa vijana kwani licha ya bingwa wa kombe hilo mshindi wa pili yeye atajishishindia Milion mbili ngao ,  jezi na mpira mmoja mshindi wa tatu Milion moja na jezi seti moja huku mshindi wa nne  kupewa laki tano.Timu zote zitakazoshiriki michuano hiyo zimekabidhiwa vifaa vya michezo ikiwa ni pamoja na jezi.

Akieleza kuhusu michuano hiyo Ummy ambaye pia ni waziri wa afya alisema kuwa kuendelea kuimarisha  afya hususani kwa vijana ni katika kuepukana na magonjwa ikiwemo yasiyo ambukiza  lakini pia kuendelea kuzalisha wachezaji wengi zaidi ambao watakwenda kuonyesha vipaji vyao katika timu mbali mbali za ndani na nje.

"Malengo zaidi ni kuwaunganisha vijana katika kata zetu zote 27 lakini pia kulinda afya zetu  tunafahamu watu wenye ugonjwa wa Moyo wanazingatia mazoezi na wanaishi vizuri lakini lengo la lingine ni kukuza na kuibua vipaji ili na sisi tuweze kutoa wachezaji wenye vipaji tumeona tuweke zawadi nono ili tuweze kuvutia vijana wengi zaidi wajitokeze kwenye michezo" 

"Mshindi wa kwanza ataondoka na shilingi milion tatu, kikombe , jezi na mipira miwili mshindi wa pili ni zawadi milion mbili , ngao  jezi na mpira mmoja  mshindi wa tatu itakuwa ni milion moja pamoja na jezi lakini tumeona tuweke na mshindi wa nne naye tapata tu laki tano hatapewa jezi wala kikombe " alisema Ummy.

Athuman Sheria ambaye ni mwenyekiti wa michezo kata ya Mabawa na mjumbe wa kamati iliyoundwa kwaajili ya ligi ya kombe la Odo Ummy Cup alisema " tunamshukuru sana nakumpongeza mbunge wetu ambaye ni waziri wa afya kwa kuanzisha wazo hili na kulitimiza, tunafurahi na tunaamini mambo yatakuwa ni mazuri zaid" 

Post A Comment: