Muonekano wa jengo la Uhamiaji mkoani Lindi.


Na Said Hamdani, LINDI.

BARAZA la wazee wa Chama cha ACT Wazalendo (ACT) Mkoa  wa Lindi limevunja ukimya na kuipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi,kuwekeza majengo ya Ofisi na kitega uchumi kwa Mji wa Lindi.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Khalfani Zaidi ametoa pongezi hizo,alipokuwa anasalimia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika viwanja vya kituo cha Afya mjini hapa.

Akisalimia wakazi hao, Zaidi amesema kazi ya upinzani sio kulaumu serikali iliyopo madarakani pale inapokosea bali ni pamoja na kupongeza inapofanya vizuri kwa wananchi inaowaongoza.

Zaidi amesema kitendo cha wizara ya Mambo ya ndani ya nchi kujenga Ofisi Idara ya Uhamiaji na kitega uchumi kwa Jeshi la Polisi ni cha kupongezwa na Jamie inayopenda Mandeleo ndio maana ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi wameamua kuipongeza wizara kwa kuliona hilo.

"Haya mawili yaliyofanywa na wizara kujenga majengo mawili ndani ya mji wetu,tunaipongeza kwa asilimia 40%"Alisema Zaidi.

Mwenyekiti huyo alisema Duniani hakuna Serikali inayofanya mazuri peke yake bila yapo na mabaya,ndio maana tunaamua kuipongeza kwa hili iliyolifanya wizara ya mambo ya ndani ndani ya mji wa Lindi.

Aidha,mwenyekiti huyo Baraza la wazee ameutaka uongozi wa Wizara hiyo kuwakumbuka Askari wake kuanzia Jeshi la Polisi,Magereza,Uhamiaji na Zimamoto kuhakikisha wanawajengea Nyumba za kuishi.

Zaidi amesema kazi zinazofanywa na Askari ni ngumu,hivyo upo umuhimu na wao wakapatiwa nyumba nzuri za kuishi.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: