Na. Anangisye Mwateba-Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki ( Mb) amekagua jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii lililojengwa kwenye mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katika ukaguzi huo aliambatana na Naibu wake Mhe. Dunstan Kitandula na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi amesema kwamba jengo hilo kwa sasa limekamilika kwa asilimia 99.9 na kwamba yamebaki maboresho madogo ambayo yatakamilika ndani ya muda mfupi.
Jengo hilo la ghorofa tano limejengwa kwa muda wa miezi 21, na limeshakaguliwa vyombo mbalimbali vya kupima ubora kama OSHA na Zimamoto.
Mhe. Kairuki ameipongeza Menejimenti ya wizara kwa usimamizi makini na kuweza kukamilisha jengo kwa haraka na ubora wa hali ya juu.
Post A Comment: