Mstahiki Meya Ibrahimu Mwangwada limepiga marufuku watendaji wa kata kuwatoza fedha wananchi wanaoenda kupata huduma ya barua pamoja na muhudi.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

BARAZA la Madiwani Manispaa ya Iringa likiongozwa na Mstahiki Meya Ibrahimu Mwangwada limepiga marufuku watendaji wa kata kuwatoza fedha wananchi wanaoenda kupata huduma ya barua pamoja na muhudi.


Akizungumza leo katika mkutano wa kata kwa kata uliofanyika kata ya Mivinjeni Mstahiki Meya huyo ameonyesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watendaji kuwatoza malipo wananchi.


Mwangwada amesema 'kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi  wakilalamikia kitendo cha kulipishwa fedha kiasi cha Tsh.10000 kwa barua na Tsh.5000 kugongewa muhuri kwenye barua  kwani wanaofanya hivyo wanakiuka MAADILI ya kazi.


 Aliongeza kuwa kuwatoza wananchi fedha kunapelekea baadhi yao  kushindwa kupata huduma kutokana na kukosa malipo.


"Kuanzia leo ni marufuku watendaji wa kata kuwatoza wananchi fedha kwa ajili ya kupata huduma,kwani huduma za barua na muhuri  zinayolewa bure hazilipiwi.Kwa mtendaji atakaebainika atakuwa amejifukuza kazi mwenyewe"Amesisitiza.


Madiwani wanaendelea na   mkutano wa hadhara kata kwa kata wakiwa wameongozana na wataalamu.


 Lengo la mkutano huo wa kata kwa kata ni   kuwaeleza wananchi nini wamekifanya toka walipoingia madarakani pia kuelezea utekelezaji wa Ilani uliofanyika kila kata.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: