Kutokana na Kasi ya mabadiliko yaliyopo katika Sayansi na Teknolojia watanzania wametakiwa kuendana na kasi hiyo hususani matumizi ya teknolojia Ili Kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji huduma ikiwa ni pamoja na kujua aina Bora ya Teknolojia ya kuendana nayo na kujiepusha na athari zake.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Asasi za Kiraia Frances Kiwanga Katika ufunguzi wa Mkutano wa wiki ya Asasi za Kiraia uliolenga kuakisi mchango wa Asasi hizo katika mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia na matumizi sahihi ya aina ya Teknolojia pasipo kuathiri ustawi wa jamii.
"Mabadiliko ya teknolojia yanakuwa Kwa kasi Sana lakini vijana wanapaswa kuangalia namna Bora yakuweza kuya akisi bila kuathiri Jamii na ndio maana tunakuwa na mijadala kama hii kuchagua ni teknolojia Gani inafaa na ipi haifai" Amesema Kiwanga.
Kwa upande wake Mrajisi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Zanzibar Ahmed Abdulah ametoa rai kwa Asasi za kiraia kuwa mstari wa mbele katika kubeba maono ya Jamii Kwa kuwa na matumizi Bora ya Teknolojia.
"Ni jukumu letu kama Asasi kuona Jamii inachagua matumizi sahihi ya teknolojia na siyo kivingine, Matumizi yanapokuwa sahihi yanaleta mtazamo chanya kwenye Jamii"amesema
Naye Mwakilishi wa Meya wa Jiji la Arusha Isaya Doita amewataka vijana nchini kuhakikisha wanakuwa na matumizi yenye tija katika mitandao ya kijamii Kwa lengo la kujiingizia kipato Kwa namna iliyohalali.
Amewataka pia kujitahidi kujifunza namna Bora ya kuendana na Teknolojia hususani katika mitandao ya kijamii huku wakiiga mifano ya waliofanikiwa kupitia mitandao hiyo na kuahidi kuwa kama Serikali wanaendelea kutoa wito kwa vijana kufanya Mabadiliko chanya kupitia teknolojia.
Abubakari Ally ni miongoni mwa vijana waliofanikiwa kupitia teknolojia ambapo ameweza kubuni na kuendeleza mradi wa Kilimo Cha kidijitali kupitia teknolojia huku akisema ana uhakika wa kupata zaidi ya dola milioni 20 Kwa heka 22 alizowekeza katika Kilimo.
Tanzania imeendelea kushuka Kasi kufuatana na mabadiliko ya kiteknolojia,Ili kuwa na mifumo Bora yenye kurahisha utoaji huduma.
Post A Comment: