Na John Walter-Manyara 

Mfuko wa Utamaduni sanaa Tanzania umetoa wito kwa wasanii wenye sifa za kupata mkopo kutoka katika taasisi hiyo kujitokeza ili kuwezeshwa fedha au Vifaa vitakavyo wasaidia kuboresha kazizao za Sanaa ili kuendana na soko la sasa na kujiajiri kupitia sanaa na utamaduni.

Wito huo umetolewa na Bi Nyakango Mahemba Mtendaji mkuu wa Mfuko wa utamaduni sanaa Tanzania,Taasisi ambayo ipo chini ya Wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo iliyoanzishwa na Serikali kwa lengo la kuwainua wasanii ili kutengeneza kazi nzuri itakayo endana na soko la Ndani na nje ya nchi.

Bi Nyakango amesema Mfuko wa utamaduni sanaa Tanzania umelenga kutoa mikopo yenye Masharti nafuu ambapo hutolewa kwa Msanii Moja moja, Vikundi au Makampuni yanayotengeneza kazi za sanaa, ambapo mikopo hiyo huanzia laki 2 Mpaka milioni 100 na riba huku riba ya Mkopo huo ikiwani ni asilimia 9 inayotozwa katika salio la Mkopo.

Aidha Bi Nyakango ameongezakuwa Kuna aina tano za mikopo inayotolewa na Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na Sanaa za Ufundi,Sanaa Za Maonyesho pamoja Sanaa za Muziki.

Bi Nyakango ameongezakuwa ''ili mtu anufaike na mikopo yetu ni lazima awe Tanzania,awena umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, afanye kazi za utamaduni pamoja na Sanaa na vilevile anatakiwa ajisajili katika taasisi ya BASATA ambao wao ndiyo wapo kisheria katika kusimamia kazi za Sanaa pia Mwombaji anapaswa kuandika andiko la Miradi itayo elezea madhumuni na malengo ya mkopo wake'' 

Kwa upande wake Msanii wa Nyimbo za Bongo Fleva Bwa. Masinde Badi kutoka mkoa wa Manyara pamoja na wasanii waliofikiwa na kuelimishwa juu ya umuhimu wa mfuko wa utamaduni na sanaa, wameishukuru Serikali kwa kubuni na kuanzisha mfuko huo kwani utawasaidia wao katika kuongeza ufanisi na ubora wa kazi za sanaa hapa nchini jambo litakalokuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Share To:

Post A Comment: