Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameendelea na kampeni ya kuwawezesha wanawake kiuchumi Halmashauuri ya Busokelo bila kujali itikadi zao kwa kutoa majiko na mitungi ya gesi aina ya ORYX likiwa ni tamasha la pili baada ya lile la ufunguzi lilozinduliwa Tukuyu Jimbo la Rungwe.

Washindi watano wamepatiwa mtaji wa shilingi elfu thelathini ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa mafunzo chuo cha VETA Mbeya ili kuboresha kiwango ili biashara ifanyike kwa ufanisi zaidi.

Tamasha litaendelea Wilaya ya Kyela na washindi wa kwanza katika halmashauri zote watanufaika na mafunzo yatakayotolewa VETA.

Hata hivyo Mahundi ametoa majiko 21 ya ziada kwa wanawake waliotoka mbali ingawa hawakupata fursa ya kushiriki tamasha.

"Kiu yangu ni kuwatumikia wanawake bila kujali itikadi zao sanjari na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan"alisema Mahundi.









Share To:

Post A Comment: