Maji si sehemu ya kundi la chakula lakini maji yana umuhimu kubwa sana kiafya katika kufanikisha kazi mbalimbali mwilini. Pia viungo vingi vya mwili ili iweze kufanya kazi vizuri vinahitaji maji na zaidi ya asilimia 60 ya uzito wa mwili wa binadamu ni maji. Hivyo maji husaidia mwili kufanya kazi mbalimbali.

Ukame na majanga mengine yanayohusiana na maji yanaongezeka kwa kasi kubwa sana nchini Tanzania kutokana na mabadiliko ya tabianchi na, ukizingatia ongezeko la idadi ya watu duniani na kupungua kwa upatikanaji wa rasilimali hiyo katika maeneo mengi huku idadi ya watu wanaoathirika na matukio haya inaongezeka.

Mabadiliko ya Tabia Nchi yamesababisha mabadiliko ya mvua kimataifa na kikanda kwa sababu ya ongezeko la joto duniani yanabadilisha mwelekeo wa mvua na msimu wa kilimo, na kuathiri uhakika wa chakula na ustawi wa binadamu.

Jumla ya maji yote ya juu ya uso wa dunia na katika chini ya ardhi, ambayo ni pamoja na barafu, yamepungua kwa sentimita moja kila mwaka katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita huku hali ikizidi kuwa mbaya kwani asilimia 0.5% ya maji hayo ndiyo yanaweza kutumika kama maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Ili kufanikisha ustawi wa muda mrefu wa kijamii, uchumi na mazingira duniani kunahitajika usimamizi jumuishi wa rasilimali za maji.Lakini nchi 107 duniani kote haziko kwenye njia sahihi kufikia lengo la kusimamia rasilimali zao za maji endelevu ifikapo 2030.

Samwel Myovela ni mkazi wa kata ya Lengijave ambapo amesema kuwa kutokana na shida ya maji hakuna maendeleo yeyote ambayo wanafanya kutokana na muda mwingi kutumia kutafuta maji kwani hata yaliyopo kwenye chazo nayoi bado ni tatizo kuyapata licha ya kutokuwa na usalama wa kutosha.

"Kero ya maji ni ya muda mrefu katika kata yetu na kusababisha wananchi wengi kutumia muda mwingi kwenda kufuata maji,Sisi wananume tunaamka kuwahi kupeleka mifugo malishoni ila wakina mama wakitoka kufuata maji inabidi wawahi minadani" alisema

"Hapa tulipo hatuelewi hatma yetu ni nini kwani maji tunayotumia ni hatari sana kwa afya zetu hebu kwani maji ya huku kama unavyofahamu yana chloride ndio maana umeona baadhi ya familia watoto wao wanachangamoto ya ulemavu" Aliongezea.

Kwa upande wake Meneja wa Usambazaji wa Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Arumeru Mhandisi Sabiri Waziri amesema mwazoni wa mwezi wa pili mwaka huu mkandarasi amepatikana na kukabidhiwa eneo la ujenzi (site) mwezi wa tatu ambapo amepewa mkataba wa mwaka mwaka kuhakikisha Kijiji cha Engalaoni sambamba na vijiji vya jirani vinapata huduma ya maji inawafikia.

“Mkandarasi yupo eneo la ujenzi na ameshaanza kazi na kwa sasa anaendelea kumwaga malighali (material) ka ajili ya ujenzi wa tanki na malighafi mengine kwa ajili ya vituo vitano vya kusambazia maji” Alisema Menenja

“Serikali tumeshasikia kilio cha wananchi wa Kijiji cha Lengijave waendelee kuwa na Subira kwani tatizo la maji katika Kijiji chao litatatuliwa ila kwa sasa waendelee kupata maji hivyohivyo ila natumaini hivi sasa mvua za siku mbili hizi wataendelea kuchota maji ili mradi huu utakapokamilika wataweza kupata maji muda wote kipindi cha kiangazi na masika kwa kupitia mradi huu mpya” Alisema





Share To:

Post A Comment: