Na Joel Maduka, Geita.

Wafanyabiashara ,wananchi na makampuni Mbalimbali nchini yameshauriwa kujenga tabia ya kusaidia taasisi zinazo toa huduma za kijamii bila kujali ni taasisi binafsi kwani kufanya hivyo inasaidia jamii nzima kupata huduma bora.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni ya  Elfam  Joel Lucas wakati akikabidhi kisima mirefu kwa shule ya awali na msingi ya Kadama iliyoko Kata ya Buseresere Wilaya  ya Chato Mkoani Geita Oktoba 21,2023.

Amesema kuwa Kampuni hiyo imeamua  kusaidia shule hiyo baada ya kuona shule hiyo inafanya vizuri kitaaluma hadi kupata mtoto wa kwanza kitaifa mwaka 2018.

Amesema kuwa jamii inatakiwa kuacha imani potofu kwamba taasisi binafsi hazipaswi kusaidiwa, kwani taasisi hizo zinahitaji kusaidiwa maana zinatoa huduma zaidi kuliko faida.

Mwanafunzi scholastica Johannes na Andrew Samwel ambao wanasoma kwenye shule ya Kadama English  Medium ambao  wamesema kabla ya kisima hicho walikuwa wanatumia muda mwingi kuhangaikia maji lakini kwasasa wanapata maji kwa urahisi.

Mkurugenzi wa shule ya Msingi Kadama Leticia Pastory amesema kuwa kabla ya msaada huo shule ilikuwa inatumia gharama kubwa kusoma maji kwa magari kutoka mbali.

Aidha amewataka wadau ,makampuni na serikali kuzisaidia shule binafsi kwani zinatoa poa huduma kwa jamii na siyo kupata faida tu.

Amesema yeye binafsi anasomesha wanafunzi ishirini (20) ambao ni yatima na kutoka familia zenye mazingira magumu ,hivyo taasisi na serikali kusaidia shule binafsi ni sahihi kabisa.

Amesema kuwa kwa sasa kisima hicho kinacho tumia mfumo wa umeme, kinatoa lita 9,000 kwa siku kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo.

Share To:

Post A Comment: