Na Joel Maduka ,Geita..
Mamlaka ya mawasiliano kanda ya ziwa TCRA ,imewataka watangazaji na waandishi wa habari kufuata kanuni na miongozo inayosimamia sekta ya habari ,ikiwa ni pamoja na wamiliki wa leseni kufuata maelekezo ya leseni zao ambazo zimeainisha lugha sahihi ambazo watangazaji wanatakiwa kuzitumia pindi wanapoendesha vipindi.
Rai hiyo imetolewa na meneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya ziwa Mhandisi,Frances Mihayo wakati wa semina ya siku moja ambayo iliwakutanisha waandishi wa habari Mkoa wa Geita iliyokuwa imelenga kuwafundisha wajibu wawatumiaji wa mawasiliano pamoja na kanuni na sheria zinazosimamia sekta ya mawasiliano na Habari.
Amesema ni vyema kwa wamiliki wa Radio Televisheni na wanaotoa huduma za habari mitandaoni kufuata taratibu ambazo zimewekwa kwa mujibu wa leseni na kuacha tabia ya kutumia lugha mbili.
"Tunafanya semina kwenye mikoa ya kanda ya ziwa za kuwakutanisha waandishi kubwa zaidi ni kuwaambia na kuwapa elimu juu ya miongozo ya utangazaji lakini pia kanuni ambazo wanatakiwa kuzingatia pindi wanapoendelea na shughuli za utoaji wa taarifa mbali mbali kwa Umma"Eng Frances Mihayo Meneja wa TCRA Kanda ya ziwa.
Kwa upande wake Muwezeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Edwin Soko amewataka waandishi wa Habari kuzingatia suala la maadili pindi wanapotekeleza majukumu yao huku akisisitiza kwa waandishi kupenda kusoma sheria na kanuni mbali mbali ambazo zinatungwa kwaajili ya kuboresha tasinia ya uandishi wa Habari.
"Niwaombe sana ndugu zangu waandishi wa Habari mnatakiwa kusoma na kujiendeleza kwa nia ya kujua masuala mbali mbali ambayo yatawasaidia kuwa huru kwenye shughuli zetu za kihabari"Edwin Soko Mwenyekiti wa MPC.
Post A Comment: