Wadau Mbalimbali wanaotumia  huduma zitokanazo na Teknolojia wameomba  Taasisi za Fedha kurahisisha huduma hizo Kwa watu wenye ulemavu ikiwemo walemavu wa macho.

Wakizungumza katika Mkutano wa Asasi  za Kiraia (Azaki) unaofanyika mkaoni Arusha wadau hao wameomba kupatiwa mfumo shirikishi utakaowasaidia kwenye utumiaji wa Teknolojia katika maeneo Mbalimbali.

Renatusi  Rupoli ambaye ni mlemavu wa macho  kutoka Iringa amesema   watu wasioona huwa wanatumia  mitandao kwa njia ya sauti ambapo alihoji kwanini kusiwepo na Software  kama hizo  ambazo zinajumlishwa  kwenye Mashine za Kutolea pesa (ATM)  Benki    Ili  kupunguza  usumbufu wakutafuta wasaidizi wakati wa kutumia huduma hizo.

Mtoa mada katika  Mkutano huo Amali Baziadi kutoka Benki ya Stanbic  amesema changamoto hiyo ameichukua na kwamba wataona namna gani yakulifanyia kazi ili kupata ufumbuzi.

"Ninaimani kuwa siyo tu Stanbic pekee ambao hatuna huduma hii lakini naichukua kama changamoto na tuone namna gani tunaifanyia kazi ili kuwawezesha wateja wetu kupata huduma rafiki kwao"amesema Baziadi.

Washiriki wa Mkutano huo wameendelea kushauri kuwepo kwa huduma rafiki Kwa wazee na wananchi waishio Vijijini namna ambavyo wanaweza kufungua akaunti za Benki kwa kutumia mitandao badala ya kufuata huduma hizo kwa mawakala wa Benki ambao mara nyingi hupatikana mijini.

Mkutano huo ulianza mapema wiki hii ambapo ASASI za kiraia zimeangazia zaidi matumizi sahihi ya teknolojia Kwa Jamii  ambapo washiriki wamkutano huo wametikea katika mashirika Mbalimbali yasiyo ya kiserikali, na wadau Mbalimbali wa Teknolojia.



Share To:

Post A Comment: