Na Janeth Raphael -Dodoma

Imeelezwa kuwa Taasisi ya Montessori Community of Tanzania (MCT) ina mbinu za Ufundishaji zinazowaandaa watoto kuwa na ujasiri na uwezo wa kujitegemea pamoja na kuishi katika Mazingira ya hali yoyote ile.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sarah Kiteleja ameyasema hayo Oktoba 5,2023  Jijini Dodoma wakati wa  Kilele Cha Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lililoenda   sambamba na Uzinduzi wa Mfumo wa Ramani wa kidijitali wa utambuzi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini.

Sarah amesema wanafanya kazi kwa karibu na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Maendeleo ya Jamii kutatua changamoto ya Kusoma,Kuandika na Kuhesabu.

Amesema kupitia vifaa vya Montessori  wameanza kufundisha mtoto kusoma,kuandika na kuhesabu.

Amesema kwenye hesabu wanafundisha msingi wa hesabu na kumwelewesha mtoto kwa kugawanya,kujumlisha na kuzidisha na kufanya hesabu mpaka 1999.

Amesema kupitia mfumo huo unamsaidia mtoto kuwa na ujasiri uwezo wa kujitegemea,kuishi mahali popote katika mazingira yoyote.

"Montessori inampatia mtoto life skills ambazo zitamsaidia kuishi popote,"amesema Bi.Sarah

Amesema wameweza kufanya utafiti kuangalia mbinu hiyo ya ufundishaji na imeleta faida gani katika Jamii.

"Katika utafiti huu imeonekana kwamba Montessori inaibua vipaji kuweza kuwa na ujuzi na kujiamini na uwezo wa kufanya vitu vipya," amesema 

Hata hivyo amesema mipango ya Shirika ni kuanza kufundisha walimu wa shule za msingi katika Chuo cha Mwanza ambapo kozi inatarajia kuanza Januari mwakani.

"Lakini pia mipango mingine tumeanza utafiti katika Mkoa wa Bukoba kwa ajili ya kuwafundisha walimu wa Serikali ili waweze kuyamudi madarasa yao"amesema Sarah

Pia amesema wana  vyuo 7 vya Montessori na tumefanikiwa kufundisha zaidi ya walezi 5000 na kuanzisha vituo vya malezi 2500 nchi nzima.

Amesema kupitia vituo vya malezi wamefanikiwa kufundisha watoto zaidi ya 100,000.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Montessori Community of Tanzania (MCT) akielezea jambo mbele ya Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango leo jijini Dodoma wakati wa kilele Cha jukwaa la mwaka la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Montessori Community of Tanzania ( MCT) Sarah Kiteleje akizungumza na Michuzi Tv leo jijini Dodoma
Share To:

Post A Comment: